-
Notifications
You must be signed in to change notification settings - Fork 0
Expand file tree
/
Copy pathtest.json
More file actions
48 lines (48 loc) · 163 KB
/
Copy pathtest.json
File metadata and controls
48 lines (48 loc) · 163 KB
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
[{"body": ["Taharuki imezuka juzi katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Wananchi (Cuf) baada ya wafuasi wanaodaiwa kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kupita katika mkutano wa chama hicho na kutoa matangazo ya uzinduzi wa kampeni za CCM zinazofanyika leo.", "\r\n", "\r\nTukio hilo lilimlazimisha mgombea urais wa Zanzibar kupitia Cuf, Maalim Seif Shariff Hamad, kukatisha hotuba yake na kuwatuliza wafuasi wake waliokuwa wakiwazomea wafuasi wa CCM wakati wakitangaza matangazo hayo.", "\r\n", "\r\nKufuatia tukio hilo, mkutano huo ulikatishwa na kusababisha wafuasi na wananchi waliiohudhuria mkutano huo kuondoka kwa kuhofia usalama wao.", "\r\n", "\r\nMapema, mgombea huyo alisema endapo atakuwa rais wa Zanzibar ataimarisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa.", "\r\n", "\r\nAlisema serikali hiyo itakuwa na uwiano wa uongozi kati ya vyama viwili vitakavyoiunda kuanzia ngazi ya juu hadi chini zikiwemo nafasi ya masheha (viongozi wa mitaa).", "\r\n", "\r\nAidha, alisema viongozi wa serikali kama makatibu wakuu hawataruhusiwa kuingia katika siasa kama ilivyo sasa.", "\r\n", "\r\nAlisema serikali atakayoiongoza, itatenda haki kwa watu wote bila kujali dini, rangi, ukabila na itikadi za kivyama na kudumisha amani ya nchi ili kuleta maendeleo.", "\r\n", "\r\n\u201cChini ya serikali nitakayoiongoza nitahakikisha najenga umoja na kutenda haki sawa kwa watu wote bila ya upendeleo,\u201d alisema.", "\r\n", "\r\nAlisema hatomvumilia mtu yeyote\u00a0 atakayejaribu kutaka kuvunja mariadhano ya serikali ya umoja wa kitaifa na anakae thubutu kufanya hivyo atakiona cha moto.", "\r\n", "\r\nNaye Mkurugenzi wa mawasiliano wa timu ya ushindi ya chama hicho, Ismail Jussa Ladhu,\u00a0 akizungumza na waandishi wa habari jana, alilaani kitendo kilichofanywa na wafuasi wa CCM cha kukatisha hotuba ya mgombea urais wa Cuf wakati akiwa katika mkutano huo.", "\r\n", "\r\nAlisema kuwa kitendo hicho cha wafuasi wa CCM kupitia katika eneo hilo la mkutano na kutoa matangazo ya uzinduzi wa kampeni wa CCM alikiita ni kitendo cha uchochezi.", "\r\n", "\r\n\u201cWamefanya makusudi inakuaje wapite tulipo sisi na kutoa matangazo yao wakati njia zipo nyingi za kupita hiki tunakiita ni kitendo cha hujuma na uchochezi,\u201d alisema.", "\r\n", "\r\nAidha, alisema kitendo hicho kilichofanywa na CCM ni kukiuka maadili ya uchaguzi ambayo walikubaliana na kuyasaini mbele ya tume ya uchaguzi.", "\r\n", "\r\nAlisema muongozo wa maadili ya uchaguzi umeweka bayana kwa vyama vya siasa kuacha kufanya vitendo vya uchochezi."], "byline": ["Na Rahma Suleiman\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Mkutano wa Seif wavamiwa na CCM"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84269", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:50.291392"},
{"body": ["Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ameibomoa \u2018ngome\u2019 ya vyama viwili kati ya vinne vinavyounda Ukawa, baada ya kuwapokea makada 47 waliojiunga na chama hicho wakitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF, mkoani Pwani.", "\r\n", "\r\nKati ya waliotimka na kujiunga na CCM, yumo Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Wilaya ya Kibaha, Grayson Nyakarungu ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya mkakati wa ushindi katika jimbo la Kibaha Mjini, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.", "\r\n", "\r\n\u201cMimi kama mama, nina huruma na ndo maana nimewapokea na kuwapa kadi za CCM. Mmewasikia vijana hawa namna walivyotumika kuijenga Chadema lakini hawakuthaminiwia\u2026Nyakarungu na wenzao mlioamua kuhamia kwenye safari ya ushindi ya Dk. John Magufuli nawakaribisha sana,\u201dalisema Samia.", "\r\n", "\r\nAkizungumza muda mfupi baada ya kujiunga na CCM, Nyakarungu alisema: \u201cNimechoshwa na siasa zinazoegama upande mmoja. Dk. Slaa kama hakusikilizwa alipoeleza msimamo wake, mie nani ataniskiliza na kunipa mwongozo. Nimekimbia Chadema kwa sababu viongozi wake wa kitaifa wameacha ile misingi ya mabadiliko na kujikita kwenye harakati za kifisadi,\u201d", "\r\n", "\r\nKatika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Kibaha stendi; mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini (CCM), Sylivester Koka alimwomba Samia kufikisha ombi maalum kwa Dk. John Magufuli\u00a0 aipandishe hadhi Hospitali ya Tumbi-Kibaha, kuwa Hospitali ya Rufaa ya mikoa ya Kanda ya Mashariki, iwapo Watanzania watakipigia kura chama hicho na kuunda serikali.", "\r\n", "\r\n\u201cHospitali ya Tumbi ambayo imekuwa mkombozi mkubwa kwa taifa, kutokana na kuhudumia wagonjwa na majeruhi wa ajali za barabarani, kutoka mikoa mbalimbali nchini, haina ICU (chumba cha uangalizi maalum), CT- Scan, vifaa tiba na madaktari bingwa. Tunakuomba mheshimiwa Samia na Dk. Magufuli muitupie macho hospitali hii,\u201dalisema Koka. ", "\r\n", "\r\nAliongeza kuwa hospitali hiyo ina upungufu wa madaktari 11, ambapo waliopo ni sita. Changamoto nyingine ni ucheleweshwaji wa madawa kutoka Bohari Kuu ya Madawa (MSD).", "\r\n", "\r\nHospitali hiyo, inayosimamiwa na Shirika la Elimu Kibaha, inahudumia wagonjwa 300 hadi 400 kwa siku, na ina vitanda 254 tu vya kulaza wagonjwa."], "byline": ["Na Godfrey Mushi\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Samia abomoa ngome ya Ukawa"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84271", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:51.315309"},
{"body": ["Mgombea urais wa chama cha Labour Party (TLP), Maxmillian Lyimo, ameungana na Edward Lowassa, kuainisha elimu kuwa ndilo suala la kipaumbele kikuu iwapo akichaguliwa kuongoza nchi.", "\r\n", "\r\nLowassa anayegombea\u00a0 kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa tiketi ya Chadema, ameeleza mara kadhaa katika kampeni zake kuwa kuboresha elimu na kuwapa Watanzania elimu bora ni kipaumbele cha serikali yake.", "\r\n", "\r\nAkizundua kampeni za urais mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Jana, pamoja na elimu, Lyimo aliahidi kudumisha\u00a0 amani, umoja na mshikamano.", "\r\n", "\r\nMgombea huyo aliyezindua kampeni na idadi ndogo washabiki\u00a0 kupindukia, alitabiri\u00a0 kuwa, uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa kihistoria lakini bila kutoa maelezo na kwamba atakayepeperusha bendera ya taifa, atakuwa shujaa atakayerudisha heshima ya shujaa, Mwalimu Julius Nyerere.", "\r\n", "\r\nAlisisitiza kuwa, awamu ya tano inatakiwa kumpata kiongozi mwenye hekima na busara akijielezea kuwa yeye\u00a0 ni\u00a0 mjumbe wa amani na aliyefunuliwa mengi akigusia kuwa miongoni mwa aliyoonyeshwa ni tukio la Julai 10 mwaka huu\u00a0 la baadhi ya wagombea\u00a0 kukatwa kwenye Halmashauri Kuu ya CCM na kuhamia upinzani.", "\r\n", "\r\nHata hivyo aliwaonya waliohama kuwa :- \u201cHuwezi kubomoa mfumo kama upo ndani yake, hawa wamekuja upinzani kubomoa chama walichokijenga ila\u00a0 swali la kuwauliza ni hili wanatuachaje?\u201d alihoji.", "\r\n", "\r\nAkizungumzia amani aliyataka madhehebu yote kuliombea taifa ili livuke salama kwa sababu lipo hatarini kuliko miaka\u00a0 iliyopita lakini akidai kuwa miongoni mwa wagombea nane wa urais yupo mfano wa Mfalme Daudi anayetajwa kwenye vitabu vya dini aliyemuita\u00a0 Nyerere wa pili.", "\r\n", "\r\n\u201cKiongozi ajaye ni lazima awe mche Mungu, mwenye\u00a0 elimu, vipaji vya ziada, maono mapya, siasa unganishi na atakayeliunganisha taifa,\u201d alisema na kuahidi kuwapa viongozi wa dini kipaumbele badala ya kuwapendelea\u00a0 wabunge wanaotembelea mashangingi.\u00a0 ", "\r\n", "\r\nPamoja na kuwapo mihimili mitatu\u00a0 mgombea wa TLP alitangaza neema kwa wanahabari akisema ataongeza mihimili zaidi ambayo ni uandishi wa habari, dini, bunge, mahakama, na serikali.", "\r\n", "\r\nAliongeza kuwa, bunge litakuwa la mseto ambapo litaweka viti 50 au zaidi kwa makundi maalum lakini pia aliponda mbio za\u00a0 mwenge kuwa ni laana na kuahidi\u00a0 kuzikomesha akichaguliwa kuongoza nchi.", "\r\n", "\r\nAkizungumza kwenye uzinduzi huo Katibu Mkuu\u00a0 wa TLP , Nancy Mrikaria ambaye ni mgombea ubunge jimbo la Temeke, alisema atahakikisha kuwa nusu ya ushuru unatozwa jimboni unabaki kwenye halmashauri ili zijiendeshe.", "\r\n", "\r\nKwa upande wake\u00a0 Naibu Katibu Mkuu ,\u00a0 Dominata Ruchungura, aliinadi ilani ya chama hichi na kueleza kuwa inalenga kutatua changamoto za afya, elimu na shida za Watanzania."], "byline": ["Na Romana Mallya\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Mgombea urais TLP aipa elimu kipaumbele"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84270", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:51.668698"},
{"body": ["Baraza la Waislamu Tanzania(Bakwata) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wamesema hadi sasa hakuna taarifa ya kuwapo kwa Mtanzania aliyepoteza maisha na wanaendelea kufuatilia na kuhakikisha kuwa mahujaji waliokwenda kuhiji Makka nchini Saudi Arabia wako salama.", "\u00a0", "Aidha, Watanzania wametakiwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki na kuwaombea dua wale wote waliopoteza maisha kutokana na mahujaji 107 kupoteza maisha nchini humo baada ya kuangukiwa na mashine ya ujenzi.", "Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubeir ndiye aliyetoa taarifa hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.", "\u00a0", "\u201cMahujaji kutoka Tanzania waliwasili huko tangu Septemba 9 mwaka huu, lakini tukio hili limetokea siku chache kabla ya ibada kuanza na idadi ya watu waliopoteza maisha na kujeruhiwa ni kubwa...hadi sasa kwa taarifa tulizo nazo hakuna Mtanzania aliyepoteza maisha,\"alisema Mufti Zuber.", "\u00a0"], "byline": ["Na Waandishi wetu \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Mufti awatoa hofu Watanzania."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84292", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:51.884120"},
{"body": ["Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (pichani), amesema hakuna mwananchi wa Kigamboni atakayepokonywa ardhi yake ili kupisha utekelezaji wa mpango kabambe wa mji mpya.", "\u00a0", "Badala yake, amesema kila mwananchi mwenye eneo lake ataruhusiwa kuendeleza maeneo yao kulingana na mpango, kuingia ubia na waendelezaji wengine na kuuza ardhi yao kwa bei ya soko na wanunuzi kuiendeleza kulingana na mpango.", "\u00a0", "Aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa mpango kabambe wa mji mpya wa Kigamboni.", "\u00a0", "Lukuvi alisema maeneo yatakayopitiwa na miundombinu na huduma za kijamii, yatatwaliwa na serikali na wananchi kulipwa fidia kwa stahili kwa mujibu wa sheria.", "\u00a0", "\u201cMoja ya masuala yaliyoshughulikiwa ni pamoja na kupunguza eneo la mpango kutoka hekta 50,934 hadi 6,494, kutoka kata tisa na kubaki sita. Kurekebisha matangazo ya zamani na kutayarisha matangazo mapya,\u201d alifafanua.", "\u00a0", "Aliyataja matangazo hayo kuwa ni namba 257 na 258 ya Julai 17, mwaka huu na tangazo namba 301 la Julai 24, mwaka huu na mchakato wote ulifuata misingi ya utawala bora kwa njia ya ushirikishi na ushirikishwaji wa wadau."], "byline": ["Na Salome Kitomary\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Waziri Lukuvi awaondoa hofu wakazi Kigamboni."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84294", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:53.364991"},
{"body": ["\u00a0", "Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, pamoja na makada wengine wa chama hicho, wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga, Mohamed Mtoi (39), aliyefariki dunia juzi usiku kwa ajali ya gari.", "\u00a0", "Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, mazishi hayo yanatarajiwa kufanyika leo saa 7:00 mchana katika kijiji cha Mkuzi Kwekingo wilayani Lushoto.", "\u00a0", "Alisema ajali hiyo ilitokea juzi usiku wakati marehemu akiwa kwenye gari lake akitokea kwenye kampeni akirudi nyumbani kwake.", "\u00a0", "UTATA WAGUBIKA", "Makene alisema Mtoi ambaye pia alikuwa Mkuu wa kanda mbalimbali za Chadema nchini, alifariki dunia wakati akipata matibabu hospitalini baada ya ajali kutokea.", "\u00a0", "\u201cMara baada ya ajali kutokea, hakuwa na majeraha yoyote bali alionekana mwenye mawenge na alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali,\u201d alisema.", "\u00a0", "\u201cBahati mbaya alipata ajali akiwa kwenye gari yeye na dereva aliyetoka naye huku makao makuu yetu Dar es Salaam na dereva aliyekuwa anamuendesha wakati wa ajali ambaye hata hivyo, hatumfahamu kwani alikuwa akifahamiana na marehemu pekee,\u201d alisema Makene.", "\u00a0", "Alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa dereva ambaye alikuwa naye, baada ya ajali hiyo kutokea, kijana ambaye alikuwa akiendesha gari hilo hakuonekana.", "\u00a0", "\u201cAmetueleza kuwa mpaka ajali inatokea mtu huyo ndiye alikuwa anaendesha gari hilo, lakini baada ya ajali kutokea hakumuona,\u201d alisema.", "\u00a0", "Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Zuberi Mwombeji, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kumtaja dereva wa gari hilo kuwa alikuwa ni Miraji Nuru (43).", "\u00a0", "Kamanda Mwombeji alisema Nuru amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto akiendelea na matibabu.", "\u00a0", "Alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na hivyo dereva gari likamshinda na kutumbukia bondeni.", "\u00a0", "\"Ndani ya gari walikuwapo hao wawili tu ambapo baada ya kutumbukia walikimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa matibabu na ndipo saa 7:00 usiku Mohamed alipoaga dunia,\" alisema Kamanda Mwombeji.", "\u00a0", "Hata hivyo, alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kujua chanzo halisi cha ajali hiyo.", "\u00a0", "Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jimbo la Lushoto kupitia Chadema, Dickson Shekivuli, alisema chama hicho kimepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa hasa kwa kuzingatia kuwa juzi ilikuwa ndiyo uzinduzi wa kwanza wa kampeni za ubunge kupitia Ukawa.", "\u00a0", "Shekivuli alisema marehemu alifanya mkutano wake wa kampeni kwa mara ya kwanza katika kata ya Mlola tarafa ya Mlola wilayani Lushoto saa 9:00 alasiri mpaka saa 12:00 jioni.", "\u00a0", "Naye Msemaji wa familia, Salim Shemng'ombe, ambaye ni kaka wa marehemu, alisema taratibu za mazishi zinaendelea ambapo wanatarajia maziko kufanyika leo kijijini kwao Mkuzi.", "\u00a0", "Kwa mujibu wa Shemng'ombe, marehemu ameacha mke na watoto wawili.", "\u00a0", "Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Lushoto, Jumanne Shauri, ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, alisema tayari wameiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec ) ili kupata mwongozo kuhusiana na kifo cha mgombea huyo."], "byline": ["Na Lulu George\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Ukawa wapata pigo."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84284", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:53.873506"},
{"body": ["Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amemrushia vijembe Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (Cuf), Maalim Seif Sharif Hamad, kwamba hana hoja ya kudai kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)haijafanya lolote kwa kuwa naye alikuwa ni sehemu ya serikali hiyo.", "\u00a0", "Rais Kikwete amesema takriban nusu ya Baraza la Mawaziri wa SMZ walitokana na Cuf, hivyo Maalim Seif hana sababu ya kutoa lawama kwamba SMZ haijafanya maendeleo yoyote Zanzibar.", "\u00a0", "\"Si Makamu wa Kwanza wa Rais? Na kama aliona haridhishwi si angejiuzulu? alihoji Rais Kikwete alipokuwa akihutubia mkutano wa ufunguzi wa kampeni wa chama hicho visiwani Zanzibar jana na kuongeza kwamba hajawahi kuona umati mkubwa kiasi kile visiwani humo tangu awe madarakani.", "\u00a0", "Alisema wanaosema Zanzibar hakuna maendeleo, siyo kweli kwani maisha ya Wazanzibari sasa yamebadilika siyo kama miaka iliyopita.", "\u00a0", "Aidha, Rais Kikwete alishangazwa na umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza jana kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni katika viwanja vya Demokrasia visiwani humu jana.", "\u00a0", "\u00a0\u201cWallah sijawahi kuona watu wengi kiasi hiki kwenye uwanja huu.! Tumeshinda hatujashinda? Shein Rais au siyo Rais na \u00a0wengine ni wasindikizaji.\u201d alisema na kuhoji Rais Kikwete.\u201d\u00a0", "\u00a0", "Alisema kwa jinsi alivyouona umati huo mkubwa kiasi hicho, ni ishara tosha kuwa Dk. Shein tayari ameshashinda anachosubiri ni kuapishwa tu.", "\u00a0", "\u201cUsione vyaelea ujue vimeundwa na muundani ni CCM, nchi ina amani, Zanzibar imetulia,\" alisema.", "\u00a0", "Rais Kikwete alisema uvumilivu na utulivu ni uongozi mzuri wa CCM na kwamba hata wanavyoongea kwenye majukwaa wanaonyesha siyo watulivu wala wavumilivu, hivyo wasipewe nafasi.", "\u00a0", "Akimwelezea mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk. Ali Mohammed Shein, alisema ni mtu makini na siyo mpole ndiyo maana anafanya maamuzi magumu.", "\u00a0", "\u201cKama kuna kipindi Dk. Shein alipata wakati mgumu wa uongozi wake ni kutokana na usumbufu wa wapinzani,\u201d alisema Rais Kikwete.", "\u00a0", "Aidha, Rais Kikwete alisema wapo viongozi walioingia madarakani, lakini hupata kigugumizi cha kutaja neno `Mapinduzi.'", "\u00a0", "Hata hivyo, Rais Kikwete alisema uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni wa tofauti kwa kulinganisha na miaka mingine na kuufananisha na mchezo wa mpira wa kukabana.", "\u00a0", "\"Kama ni mpira mwaka huu, ni man to man. Tunatakiwa kuhakikisha tunakuwa makini na kuhakikisha chama kinapata ushindi kwa kupiga kura,\u201d alisema.", "\u00a0", "Aliwataka wafanye kampeni za nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba na shuka kwa shuka mpaka wahakikishe Dk. Shein anaingia Ikulu.", "\u00a0", "Kuhusu kauli ya Malim Seif kuwa upinzani upewe siku 100 \u00a0kuhakikisha wanashughulikia suala la haki ya Zanzibar kumiliki rasilimali zake za mafuta na gesi, Rais Kikwete alisema jambo hilo tayari ni ajenda ya serikali.", "\u00a0", "Alisema serikali ilijitahidi kutafuta wanasheia wawili ambao walipitisha sheria nzuri za umiliki wa mafuta na gesi baada ya Bunge kupinga suala hilo.", "\u00a0", "SHEIN KUENDELEA KULINDA MUUNGANO", "Kwa upande wake, Dk. Shein alisema ataendelea kuulinda Muungano pamoja na kuyaenzi Mapinduzi pamoja na \u00a0kulinda sekta ya mafuta na gesi kwa maslahi ya Wazanzibar endapo akichaguliwa kwa mara ya pili kuingoza Zanzibar.", "\u00a0", "Kadhalika, amesema ataendelea kulinda amani iliyopo kwa kuwa bila amani, umoja na utulivu, maendeleo hayatapatikana.", "\u00a0", "Dk. Shein alisema katika miaka mitano aliyokuwa madarakani amedumisha Mapinduzi kwa kushirikiana na Marais waliomaliza muda wao wa uongozi wa Bara na Visiwani.", "\u00a0", "\u201c Tutaendeleza umoja uliokuwapo kati ya Wazanzibari na Bara kwa kuwa sote ni kitu kimoja na ni ndugu, hivyo hatuna sababu ya kubaguana,\u201d alisema Dk. Shein.", "\u00a0", "Aidha, alisema hatamuogopa mtu yeyote katika kuhakikisha amani ya nchi haipotei kwa kusimamia haki na sheria kwa kila Mtanzania.", "\u00a0", "Pia alisema atakikisha anaitetea Tanzania katika medani ya kimataifa.", "\u00a0", "UCHUMI WA ZANZIBAR", "Dk. Shein alisema uchumi wa Zanzibar umekua kutoka asilimia 5.2 mwaka 2010 na mwaka 2011 hadi asilimia 7.2 mwaka huu ikiwa ni juhudi za Serikali inayoongozwa na CCM.", "\u00a0", "MKAPA", "Rais mstaafu Benjamin Mkapa, alisema ana imani na Dk. Shein kwa kuwa amefanya naye kazi kwa muda mrefu na anamfahamu utendaji wake wa kazi kuwa ni muadilifu, mchapakazi na ni mtu anayewania maendeleo ya wananchi wote bila ubaguzi.", "\u00a0", "Alisema Zanzibar inatakiwa kuwa na viongozi watakaouenzi Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar pasipo kuwasahau waasisi na watu waliojitolea uhai kwa ajili ya taifa.", "\u00a0", "\u201c Ni fahari kwangu kuwa nina imani na Dk. Shein kuingoza tena Zanzibar kwa miaka mitano mingine ijayo kwa kuwa ataiweka Zanzibar katika mikono iliyo salama,\u201d alisema Mkapa.", "\u00a0", "MWINYI", "Naye Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, alisema Wazanzibari wanapaswa kuchagua kiongozi mwenye maslahi na taifa lake na mwenye kuileta amani Zanzibar.", "\u00a0", "Alisema Dk. Shein ndiye kiongozi anayefaa kuiongoza Zanzibar kwa kuwa anajua Wazanzibar wanahitaji nini", "\u00a0", "KARUME", "Kwa upande wake, Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, alisema Zanzibar ina historia kubwa.", "\u00a0", "Alisema mwaka 1992, ilibadilishwa Katiba ya Zanzibar na ile ya Muungano na kuruhusu mfumo wa vyama vingi nchini.", "\u00a0", "Alisema amani inayodumu Zanzibar haikuja kwa uzi wa buibui kwa kutembea, bali ililetwa na Marais waliotangulia wa CCM.", "\u00a0", "Alisema wanzibar wanapaswa kulinda amani na kuwa nchi moja kama ilivyoachwa na marais hao waliotangulia.", "\u00a0", "DK. BILAL", "Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Mohammed Gharib Bilal, alisema uongozi wa nchi umekuwa ukiongozwa na CCM tangu ilipokabidhiwa kutoka kwa wakoloni.", "\u00a0", "\"Bila ya uongozi wa CCM, nchi itakuwa matatani, bila ya uongozi wa CCM, amani itakuwa shakani na utulivu hautakuwApo pamoja na maendeleo hayatapatikana,\" alisema.", "\u00a0", "BALOZI SEIF ALI IDDI", "Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, Balozi Seif \u00a0Ali Iddi, alisema Dk. Shein amefanya mambo mengi ya maendeleo kwa kushirikiana na upinzani kwa miaka mitano iliyomalizika.", "\u00a0", "Alisema mwaka huu ni wa CCM kuishinda Cuf kwa kishindo na kwamba ni mwaka mwisho wa Cuf kushindana na CCM kiushindani.", "\u00a0"], "byline": ["Na Waandishi wetu \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Kikwete amlipua Maalim Seif."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84290", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:53.881817"},
{"body": ["Mgombea urais iliyesimamishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, \u00a0ametua katika Jimbo Singida Kaskazini la Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazoro Nyalandu, huku akiwatahadharisha wananchi wasipompigia kura za kuitosha kuiondoa CCM madarakani watakuwa wamejiangamiza.", "\u00a0", "Aidha, amwelezea Nyalandu kuwa anamfahamu mbunge huyo kwa mbwembwe na nguvu ya fedha na kuhoji kama mgombea ubunge kupitia Chadema katika jimbo hilo, David Jumbe atamuweza.", "\u00a0", "Akizungumza na mamia ya wananchi wa kijiji cha Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini \u00a0jana ikiwa ni mfululizo wa ziara zake ya kuomba ridhaa kwa wananchi wamchague awe rais wa awamu ya tano, Lowassa alisema CCM itaondolewa madarakani kama wananchi wengi watajitokeza kupiga kura ya kuikataa.", "\u00a0", "\u201cWatu wanataka mabadiliko ya maisha yao na sisi tumejitolea kuleta mabadiliko hayo,suala la kura ni muhimu sana mabadiliko yatakuja kwa kupiga kura tusipopata kura za kutosha tumeeangamia,\u201d alisema.", "\u00a0", "Lowassa ambaye hadi sasa amefanya mikutano ya kampeni zaidi 32 katika majimbo ya mikoa 11 aliyotembelea, alisema CCM imeshindwa kuleta mabadiliko ya maendeleo na maisha ya wananchi yameendelea kuwa magumu.", "\u00a0", "\u201cWakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM Nilisema huwezi kuzuia gharika kwa mkono, sasa wameona gharika ya watu, tumekwenda Mpanda, Tabora, Iringa na leo (jana) hapa kwenu hivyo hivyo watu ni wengi,\u201d alisema.", "\u00a0", "Mgombea huyo wa Ukawa aliwataka \u00a0wananchi wasikubali kura ziibwe na kutaka apatiwe kura si chini ya milioni 12 ili awe Rais.", "\u00a0", "Alisema serikali ya CCM imekuwa ikiahidi mambo mengi lakini haiyatekelezi na kwamba serikali atakayoiunda itakuwa ya vitendo kwa kutekeleza mambo yote.\u00a0", "\u00a0", "Lowassa aliahidi akichaguliwa ataanzisha viwanda \u00a0vya alizeti na vitunguu ili viwe vinasafirishwa kwenda masoko ya nje.", "\u00a0", "\u00a0KUHUSU NYALANDU \u00a0 \u00a0 \u00a0 \u00a0 \u00a0 \u00a0 \u00a0 \u00a0 \u00a0 \u00a0 \u00a0\u00a0", "Akimzungumzia Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Nyalandu, alisema anamfahamu kwa mbwembwe nyingi.", "\u201cNamfahamu Mbunge wenu wa sasa, namfahamu kwa mbwembwe zake sasa namulize Jumbe (mgombea Chadema) utamuweza maana kuna nguvu ya pesa na nguvu ya mtu,\u201d alisema.", "\u00a0", "Hata hivyo, Jumbe alijibu kuwa tayari ameshamshinda Nyalandu.", "Katika hatua nyingine wazee wa mila wa kabila la \u00a0kimasai na kinyatulu walimkabidhi Lowassa fimbo na mgolole ili aitumie kwa ajili kuwachapia wezi ili wasimzue kuingia Ikulu na kumtaka asiiache kila aendako.", "\u00a0", "MGOMBEA UBUNGE CHADEMA", "Naye mgombea ubunge wa Chadema Jimbo la Singida Kaskazini, David Jumbe, alimweleza Lowassa kuwa jimbo hilo linakabiliwa na kero za ubovu wa barabara, ukosefu wa soko la kuuzia mazao na hivyo wakulima kulanguliwa na wafanyabiashara.", "\u00a0", "\u201cMfano soko la vitunguu ikifika wakati wa mavuno wafanyabiashara kutoka Kenya wanakuja kwa wingi na kununua vitunguu na kwenda kuviuza nje kama bidhaa iliyozalishwa nchini mwao,\u201d alisema.", "\u00a0", "Alisema kama akichaguliwa, askari wote wa mgambo watapewa majembe wakalime kwa sababu kazi ya kusimama kwenye mageti kwa ajili ya kutoza ushuru haitakuwapo na miti iliyopo katika mageti hayo itageuzwa kuwa kuni. \u00a0", "\u00a0", "LISSU", "\u00a0", "Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, alisema CCM haiwezi kuleta mabadiliko yeyote na hata ahadi ya Sh. milioni 50 kwa kila kijiji ni danganya toto.", "\u00a0", "\u201c Lowassa ametukanwa na tumemsema sana lakini ukweli wa Mungu hakufanya kosa lolote binafsi na hata wanaomtukana leo ni kwa sababu ameondoka CCM na siyo kwa sababu ya kashfa ya Richmond\u201d alisema.", "\u00a0", "MASHA", "Naye aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, aliwataka \u00a0wananchi waiogope CCM, akisema \u00a0imesababisha mateso makubwa kwao.", "\u00a0", "\u201cMtakayemuona ananunua shahada za kupigia kura katika eneo lenu, makamateni, mshughulikie na mtoweni katika eneo lenu,\u201d alisema.", "\u00a0", "MGEJA", "Kwa upande wake, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, alisema wanaotoka ndani ya CCM ni watu safi na waonang\u2019ang\u2019ania ni wachafu.", "\u00a0", "\u201cTunapofanya mabadiliko tujiamini, Ikulu siyo ya Mangula wala Nape, nchi nyingi za Kiafrika zimefanya mabadiliko kwa kuviangusha vyama tawala kwanini isiwezekane Tanzania,\u201d alisema.", "\u00a0", "JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI", "Akihutubia wananchi wa mjini Kiomboi katika \u00a0Jimbo la Iramba Magharibi, Lowassa aliahidi kuwa akichaguliwa ataanzisha benki ya bodaboda."], "byline": ["Na Thobias Mwanakatwe\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Lowassa: Msifanye kosa kuichagua CCM."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84286", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:54.228313"},
{"body": ["Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amesema pamoja na vitisho ambavyo amevipata kutoka kwa mahasimu wake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hatarudi nyuma mpaka atakapohakikisha chama hicho kimeng\u2019oka madarakani.", "\u00a0", "Kadhalika, amesema mwisho wa CCM kukaa madarakani ni mwaka huu kwa kuwa wananchi wameamua kufanya mabadiliko wenyewe.", "\u00a0", "Aliyasema hayo jana wakati akizindua kampeni za ubunge Jimbo la Ubungo za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa Katiba \u00a0 \u00a0 \u00a0ya \u00a0Wananchi (Ukawa).", "\u00a0", "Alisema ukiwa ndani ya CCM, ni vigumu kufanya mabadiliko kutokana na mfumo uliopo, lakini hata mtu akiamua kwenda chama kingine kutokana na ukiritimba wa CCM, anakuchukiwa.", "\u00a0", "Alisema kwa ambavyo ametembea katika mikoa mbalimbali kwa kampeni za kitaifa za mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) anayeungwa mkono vyama shirika vya Ukawa, Edward Lowassa, CCM mwaka huu ni lazima iondoke madarakani.", "\u00a0", "Alitaja mambo manne ambayo yatachangia CCM kuondoka madarakani kuwa ni pamoja na ukosefu wa Katiba ya Wananchi ya kudhibiti utawala mbovu ambayo alisema Ukawa wakichukua dola, litakuwa jambo la kwanza kuanza nalo na itawapa wananchi mamlaka ya \u00a0kuwa watawala wa viongozi.", "\u00a0", "Nyingine ambayo alisema imewafikisha Watanzania katika hali hiyo ya umaskini kuwa ni kukosekana kwa umoja, uzalendo, uadilifu wa utawala ambao umesababisha kutowajibika kwa viongozi na hata kuacha mianya ya rushwa.", "Sumaye alisema yeye hajaenda upinzani kwa ajili ya uroho wa madaraka kama wengine wanavyodai, kwa kuwa hagombei nafasi yoyote.", "\u00a0", "Kwa upande wake, mgombea wa ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Ukawa, Saed Kubenea, alisema endapo wananchi wa Ubungo watamchagua, hawatajuta kamwe kwa kuwa amejipanga vya kutosha kuwasaidia.", "Kubenea alisema akiingia madarakani, atashughulikia tatizo la usafiri katika jimbo hilo, tatizo la maji, afya na matatizo mengine.", "\u00a0"], "byline": ["Na Elizabeth Zaya\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Sumaye: Sirudi nyuma mpaka CCM ing'oke madarakani."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84296", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:54.908281"},
{"body": ["Serikali imeshauriwa kuboresha mazingira ya upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo ya vijijini kwa kuongeza wataalamu wa afya, dawa pamoja na kujenga zahanati \u00a0ili kuboresha afya ya mama na mtoto.", "\u00a0", "Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa tathmini ya utekelezaji wa mradi wa Wazazi na Mwanza uliotekelezwa katika Wilaya za Ilemela na Sengerema mkoani Mwanza, Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa shirika la kimataifa la Plan International, Jane Mrema, alisema iwapo serikali itaboresha huduma za afya, afya za mama na mtoto zitakuwa salama.", "\u00a0", "Alisema maeneo mengi ya vijijini yanakabiliwa na ukosefu wa wataalam wa afya, dawa na ukosefu wa vituo vya afya hali inayoathiri utoaji wa huduma hizo kwa mama na mtoto. Mrema alisema mradi huo wa miaka minne, ulimalizika Machi, mwaka huu na kupata mafanikio kwa wanaume kuwashawishi kushiriki katika mradi huo.\u00a0", "\u201cKabla ya mradi, Mkoa wa Mwanza kulikuwa na asilimia 49.1 ya wanaume kutoshiriki huduma za uzazi na mtoto, lakini baada ya kuanza mradi kwa kipindi hicho tumefanikiwa kwa asilimia 68.2\u2026hayo ni mafanikio makubwa katika masuala ya afya,\u201d alisema Mrema.", "\u00a0", "Naye Meneja wa Plan International Mkoa wa Mwanza, Grace Semwaiko, alisema mradi huo ulilenga kuboresha afya ya mama na mtoto katika Wilaya za Ilemela na Sengerema. Semwaiko alisema wakati wa mradi huo, elimu katika sekta ya afya kuanzia ngazi ya familia ilitolewa pamoja na vifaa mbalimbali yakiwamo magari ya wagonjwa, boti mbili za wagonjwa katika Ziwa Victoria wilayani Sengerema na ujenzi wa chumba cha upasuaji mama wajawazito. \u201cLengo la kutoa vifaa hivyo ni kusaidia kupunguza vifo kwa mama na mtoto \u00a0ama kumalizika tatizo kabisa hususan katika wilaya hizo mbili,\u201d alisema Semwaiko. \u00a0"], "byline": ["Na Daniel Mkate\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Serikali yashauriwa kuboresha afya."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84303", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:55.258425"},
{"body": ["Utamaduni wa kuhifadhi fedha benki na taasisi zingine za kifedha, unaongezeka taratibu kwa watanzania siku hadi siku.", "\u00a0", "Hii inafanyika kwa ajili ya usalama wa fedha zao na kupata faida inayotokana na riba toka \u00a0taasisi za kifedha.", "\u00a0", "Kwa mujibu wa \u00a0Ripoti ya Utafiti ya Mwaka 2013 uliofanywa na FinScope na kuzinduliwa Aprili mwaka jana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ( BOT ) Prof. Benno Ndulu, inaonyesha Watanzania milioni 3.3 wanatumia huduma za kibenki.\u00a0", "\u00a0", "Utafiti pia umeonyesha ongezeko la Watanzania milioni 12 wanaotumia huduma za kifedha zisizo rasmi, katika kipindi cha miaka minne iliyopita \u00a0hadi kufikia mwaka jana.", "\u00a0", "Pia umeonyesha \u00a0upande mwingine kuwa, ile hali ya kuhifadhi fedha majumbani kwa baadhi ya watu bado ipo.", "\u00a0", "Asilimia 70 ya Watanzania kwa mujibu wa utafiti hu, bado wanatunza fedha zao nyumbani badala ya kwenye mfumo rasmi, yaani ule wa benki na huduma nyingine za kifedha.", "\u00a0", "Pia unabainisha kwamba, asilimia 70.4 ya Watanzania milioni 24.2 wanaostahili kupata huduma za kifedha, hawazitumii kutokana na sababu mbalimbali.", "\u00a0", "Utafiti huo uliosimamiwa na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), ulilenga kujua idadi ya Watanzania wanaofikiwa na kutumia huduma za kifedha, na namna wanavyozitumia nchini.", "\u00a0", "Pamoja na uwapo wa ongezeko la wananchi wanaotumia huduma za kibenki na za taasisi zingine za kifedha kwa ajili ya kuboresha maisha yao kama zilivyoonyeshwa kwenye utafiti huo, bado kuna eneo ambalo halijachangamkiwa vya kutosha na wananchi.", "\u00a0", "Eneo hili \u00a0kimsingi ni salama, la uhakika na lenye kuinua hali za kipato cha wananchi na taifa kwa ujumla, ni lile la kuwekeza au kuhifadhi fedha zao kwenye dhamana za serikali za muda mfupi (Treasury bills) na za muda mrefu (Treasury bonds).", "\u00a0", "Akizungumza kwenye semina ya waandishi wa habari iliyofanyika \u00a0Bagamoyo kuhusu dhamana za serikali za muda mfupi na za muda mrefu, Mkurugenzi Mshiriki wa Kurugenzi ya Masoko wa BOT Paul Maganga alisema, \u00a0eneo hilo liko wazi kwa Watanzania wote. Maganga alisema, uwekezaji huo unawafaa watu wa kada zote kuanzia wakulima wa kawaida, wastaafu, vyama vya ushirika, Saccos na wengineo wenye kiasi kinachokubalika kuwekeza.", "\u00a0", "\u201cKiwango cha chini cha kushiriki kwenye uwekezaji huu ni Sh.500,000 kwa dhamana za serikali za muda mfupi na Sh. 1,000,000 kwa dhamana za serikali za muda mrefu,\u201d alisema.", "\u00a0", "\u00a0Maganga alisema kuwa, uwekezaji huo unawafaa watu wote wenye shughuli zao za kila siku \u00a0ama za msimu, kama vile wakulima na wastaafu.", "\u00a0", "Alisema uwekezaji huu unawafaa wakulima wanapokuwa wameuza mazao yao, ama wastaafu wanaopata fedha zao kwa kipindi fulani fulani, kama vile baada ya kila miezi mitatu.", "\u00a0", "Maganga alisema, kuna tija kwa kada hii ya wananchi kuwekeza fedha zao zitokanazo na mauzo ya mazao yao, ama kiinua mgongo na pensheni zao kwenye dhamana za serikali za muda mfupi ama mrefu, kwani zitawasaidia kuishi maisha yenye mafanikio.", "\u00a0", "Ofisa Mkuu wa BOT Mohamed Kailwa \u00a0akifafanua kuhusu \u00a0dhamana za serikali alisema ni nyenzo inayotumiwa na serikali kukopa kutoka kwa wananchi wake.", "\u00a0", "\u201cSerikali inakopa kutoka kwa wananchi kwa ajili ya kupata fedha za kugharamia utekelezaji wa miradi yake mbalimbali ya maendeleo, kwa ahadi ya kuzirudisha na riba baada ya kipindi fulani, kiwe cha muda mfupi (Treasury bills) ama cha muda mrefu na za muda mrefu (Treasury bonds),\u201d alisema.", "\u00a0", "Kailwa alisema kuwa, serikali inakopa kupitia \u00a0masoko ya fedha ambayo dhamana za serikali huuzwa kwa njia ya mnada unaoendeshwa na BOT.\u00a0", "\u00a0", "Masoko ya fedha \u00a0alisema kuwa, ni kama yalivyo masoko mengine ya kawaida tofauti ni kwamba katika masoko haya, bidhaa kuu inayouzwa ni fedha.", "\u00a0", "Kailwa alisema, ununuzi wa dhamana za serikali za muda mfupi hufanywa kwa njia ya mnada unaoendeshwa na BOT kila wiki siku ya Jumatano", "\u00a0", "\u00a0\u201c Mwananchi anaweza kununua dhamana za serikali za muda mfupi unaohusisha siku 35, 91, 182, na 364.\u201d Alisema.", "\u00a0", "Mwananchi mwenye kiwango kinachoanzia Sh. 500, 000 na kuendelea, alisema kuwa anaweza kununua dhamana \u00a0za muda mfupi kwa kuchagua siku anazotaka kuikopa serikali kati ya zilizotajwa hapo juu.", "\u00a0", "\u201cDhamana za serikali za muda mfupi zinauzwa kwa punguzo kwa kila Sh. 100, kwa maana kwamba mwekezaji anapoikopesha serikali kwa mfano Sh.95 kwa kila 100, \u00a0atalipwa zote sh. 100 baada ya kuiva kwa muda wa siku alizochagua,\u201d alisema. Matokeo ya mnada hutolewa siku hiyo hiyo ya mnada kupitia tovuti ya BOT au kwenye ofisi zote za mawakala walioidhinishwa na benki hiyo.", "\u00a0", "Alisema serikali huwalipa walionunua \u00a0dhamana hizo za fedha na riba zao, baada ya kuiva kwa kipindi cha dhamana husika.", "\u00a0", "Kwa upande wa dhamana za serikali za muda mrefu, Kailwa alisema kuwa, hulipwa mara mbili kwa mwaka.", "\u201cKiwango cha fedha cha chini kuwekeza katika dhamana hizi za muda mrefu, huwa ni sh. milioni moja na kuendelea, kwa muda wa miaka miwili, mitano, saba, 10 na 15,\u201d alisema", "\u00a0", "Aidha alisema, viwango vya riba ya dhamana za muda mrefu huwa ni asilimia 7.82 kwa mwaka kwa dhamana ya miaka miwili, asilimia 9.18 kwa mwaka kwa ile ya miaka mitano, asilimia 10.08 kwa mwaka kwa ile ya miaka saba, asilimia 11.44 kwa mwaka kwa ile ya miaka 10 na asilimia 13.50 kwa mwaka kwa ile ya miaka 15.", "\u00a0", "\u201c Ninawaasa Watanzania kutumia kwa ukamilifu fursa hii ambayo bado haijafahamika na wengi ili kujiletea maendeleo yao binafsi, na kukuza uchumi wa nchi,\u201d alisema na kuendelea.", "\u00a0", "\u201cKabla ya kushiriki katika mnada, mwekezaji yeyote anapaswa kufungua akaunti ya dhamana za serikali kwa wakala atakayemchagua na kujaza fomu maalumu ya zabuni toka kwa mawakala maalumu waliosajiriwa na BOT, ambao wako katika maeneo mbalimbali nchini,\u201d alisema", "\u00a0", "Alisema, mawakala hawa wameidhinishwa kushiriki kwenye minada moja kwa moja kwa niaba yao wenyewe, \u00a0pia kwa niaba ya wateja wao.", "\u00a0", "Kailwa alisema, BOT hutoa tangazo la mnada kupitia vyombo vya habari kila siku ya Ijumaa na mawakala hujaza maelezo ya fomu kwenye mfumo maalumu wa benki hiyo uitwao Central Depository System (CDS).", "Alisema mfumo huu, hufanya mchakato na kutunza kumbukumbu za minada kielektroniki.", "\u00a0", "Kuhusu malipo kwa dhamana zilizonunuliwa na wananchi, Kailwa alisema, muda wa kuiva dhamana za muda mfupi utakapowadia, wawekezaji watalipwa asilimia 100 ya thamani ya dhamana ikiwa imejumuishwa na thamani ya manunuzi na faida.", "\u00a0", "\u201cKwa upande wa wawekezaji wa dhamana za serikali za muda mrefu, wawekezaji watalipwa faida mara mbili kwa mwaka, na faida itategemea kiwango cha riba kilichowekwa kwa kila dhamana,\u201d alisema na kuendelea.", "\u00a0", "\u201cKwanza ni salama kwa mwananchi, serikali haitarajiwi kushindwa kulipa wadai wake \u00a0dhamana zinapoiva.\u00a0", "\u00a0", "Mwekezaji anaweza kuziuza kabla ya muda wake wa kuiva kama itakuwa lazima kufanya hivyo,\u201d alisema.", "Maganga alifafanua faida nyingine kwa dhamana hizo za serikali kutolewa kama dhamana kwa ajili ya mikopo.", "\u00a0", "\u201cNi wakati muafaka sasa kwa wananchi wa kada zote kuchangamkia fursa hii kwa minajili ya kuboresha maisha yao na kustawisha uchumi wa nchi kama wananchi wa mataifa mengine wanavyofanya,\u201d alisema"], "byline": ["Na Raphael Kibiriti\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Watanzania dhamana za uwekezaji zinalipa."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=83082", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:55.469648"},
{"body": ["Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi umesema mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (Cuf), Maalim Seif Sharif Hamad, anaupotosha umma juu ya mafanikio yaliyopatikana chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na Rais, Ali Mohamed Shein.", "\u00a0", "Aidha, umoja huo umesema kauli iliyotolewa na mgombea huyo wa urais kuwa atatoa ajira kwa vijana wote wa Zanzibar katika kipindi kifundi atakapochaguliwa kuwa Rais \u00a0ni kuwarubuni na kuwadanganya wananchi ili wampigie kura.", "\u00a0", "Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na \u00a0UVCCM kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wake, Shaka Hamdu Shaka, Maalim Seif amekuwa akipotosha na kuudanganya umma kuwa serikali hiyo imeshindwa kufikia maendeleo yake tangu iundwe miaka mitano iliopita.", "\u00a0", "Shaka alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar huongwazwa kwa pamoja kati ya vyama vya CUF na CCM, hivyo madai anayotoa Maalim Seif yanalenga kutaka kupigiwa kura kuliko ukweli halisi.", "\u00a0", "Kwa mujibu wa Shaka, serikali hiyo \u00a0imetekeleza majukumu yake kwa ufanisi \u00a0kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo kama kukuza uchumi, kuboresha huduma za afya, miundombinu, utalii na elimu.", "\u00a0", "Alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Shein pia imepandisha bei ya karafuu, zao ambalo ni tegemeo kubwa kiuchumi kwa Wazanzibari wengi.", "\u00a0", "Aidha, alisema chini ya uongozi wa Dk. Shein serikali hiyo imefanikiwa kupandisha mishahara kwa watumishi wa umma mara tatu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jambo ambalo alisema ni mafanikio makubwa katika kuimarisha huduma na maendeleo ya jamii.\u00a0", "\u00a0"], "byline": ["Na Beatrice Shayo\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["UVCCM wamvaa Maalim Seif Serikali ya Umoja wa Kitaifa."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84298", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:55.973132"},
{"body": ["Magoli kutoka kwa Simon Msuva na Donald Ngoma yalitosha kuipa Yanga mwanzo mzuri wa msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuifunga Coastal Union 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa.", "\u00a0", "Ushindi umewafanya mabingwa Yanga kuhitimisha raundi ya kwanza ya mechi wakiwa kileleni mwa msimamo mwa ligi kutokana na tofauti ya magoli wakilingana pointi na washindi wa pili wa msimu uliopita, Azam, Simba, Majimaji, Toto African, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, ambazo zote zilishinda mechi za ufunguzi juzi.\u00a0", "\u00a0", "Msuva ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipatia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya nane baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa krosi iliyopigwa na Tambwe baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Coastal Union.", "\u00a0", "Yanga, ambayo ilicheza mpira wa utulivu ilimiliki mpira zaidi kwenye kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga ambapo katika dakika ya 17 Niyonzima alikosa goli baada ya shuti lake kutoka nje kidogo ya goli.", "\u00a0", "Kabla ya kukosa goli hilo, Niyonzima aligongeana vizuri na Tambwe lakini nahodha huyo wa timu ya taifa ya Rwanda alikosa umakini katika umaliziaji.", "\u00a0", "Katika dakika ya 29, Hemed Alli (Shiboli) ambaye alikuwa msumbufu kwa mabeki wa Yanga , alikosa goli baada ya shuti lake ndani ya eneo la hatari kupaa juu.", "\u00a0", "Yanga iliendelea kutawala mpira na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na juhudi zao zilizaa matunda katika dakika ya 42 wakati Ngoma alipotumia vizuri makosa ya mabeki wa Coastal Union waliozembea kuokoa mpira ulikuwa ukizagaa langoni mwao na \u00a0kupiga shuti hafifu liloingia nyavuni.", "\u00a0", "Kuingia kwa goli hilo la pili kuliwafanya wachezaji wa Coastal Union kukata tama na kushindwa kuwadhibiti viungo wa Yanga kutotawala mpira.", "\u00a0", "Mpaka timu hizo zinaenda mapumziko Yanga ilikuwa mbele kwa magoli hayo 2-0, Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku \u2018Wagosi wa Kaya\u2019 wakianza kwa kusaka goli ambalo lingewarudisha mchezoni lakini kukosa umakini kwa safu yao ya ushambuliaji kuliwakosesha magoli.", "\u00a0", "Dakika ya 55, Shiboli alikaribia kuipatia timu yake goli la kwanza lakini shuti lake kali akiwa ndani ya eneo la hatari lilitoka nje kidogo ya lango.", "\u00a0", "Shiboli alipokea pasi safi kutoka kwa mtokea benchi, Ibrahim Twaha, ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Adeyum Ahmed.", "\u00a0", "Kipindi cha pili Yanga waliendelea kuliandama lango la Coastal lakini pamoja na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, washambuliaji Ngoma na \u00a0Amis Tambwe walishindwa kuzitumia nafasi hizo na kujikuta wakikosa magoli katika dakika za 64 na 75.", "\u00a0", "Baada ya kuona kama tayari wamejihakikishia ushindi kwenye mchezo huo, Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm, alifanya mabadiliko kwenye kikosi chake kwa kumtoa Tambwe na kuingia Malimi Busungu katika dakika ya 69 na dakika nne baadae akamtoa Geofrey Mwashiuya na kuingia Deus Kaseke.", "\u00a0", "Hata hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kubadili matokeo hayo na mpaka mpira unamalizika, Yanga walitoka kifua mbele kwa ushindi huo wa magoli 2-0.", "\u00a0", "Baada ya mchezo huo, Kocha wa Yanga, Pluijm, alikili kuwa mchezo ulikuwa mgumu na Coastal Union walikuwa katika kiwango kizuri na kuwapa tabu.", "\u00a0", "Alisema kuwa Coastal walicheza mchezo wa kasi na walikuwa wepesi kukaba pindi wanapopoteza mpira huku akiwasifu viungo wa timu hiyo.", "\u00a0", "\u201ctunaangalia mbele kwa sasa, tunashukuru kwa matokeo haya japo hatukuyapata kirahisi kutokana na upinzani tulikumbana nao,\u2019 alisema Pluijm.", "\u00a0", "Yanga itashuka tena kwenye uwanja wa Taifa keshokutwa \u00a0Jumatano kukabiliana na Tanzania Prisons ambao walipoteza mchezo wao wa kwanza uliochezwa juzi dhidi ya Azam FC baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-1.", "\u00a0", "Yanga: \u00a0Ally Mustapha \u2018Bartez\u2019, Mwinyi Haji, Mbuyu Twite, Kelvin Yondani, Nadir Haroub \u2018Canavaro\u2019, Thaban Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/ Salum Telela (89), Amis Tambwe/ Malimi Busungu (69), Donald Ngoma, Geofrey Mwashiuya/Deus Kaseke (73).", "\u00a0", "Coastal Union:Sebwato Nicholaus, Hamad Juma, Yassin Mustapha, Ernest Joseph, Tumba Sued, Said Jeilan, Shiboli, Youssoufa Sabo, Nassoro Kapama, Godfrey Wambura, Adeyum Ahmed/Ibrahim Twaha (21).", "\u00a0"], "byline": ["Na Faustine Feliciane\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Yanga yaanzia kileleni bara."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84308", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:56.531672"},
{"body": ["Penye nia pana njia.\u201d Huu ni usemi maarufu na wa siku nyingi wa Kiswahili, ambao pengine maana yake katika vita dhidi ya umaskini, ni muhimu hadi leo nchini kote.", "\u00a0", "Jitihada za kupambana na umasikini zimekuwapo nchini, tangu mwanzoni mwa miaka ya uhuru. Kwa namna moja au nyingine, zimeleta mabadiliko katika maisha ya wananchi, ingawa si kwa kasi kubwa kama ilivyotarajiwa.", "\u00a0", "Takwimu zinaonyesha kuwa, takriban asilimia 33.6 ya Watanzania wanaishi katika umasikini uliokithiri wa kipato, jambo linaloendelea kuathiri ustawi wa maisha yao na hivyo kuongeza mzunguko wa umasikini miongoni mwao.", "\u00a0", "Athari za umasikini katika kaya mbalimbali za wananchi, hujidhihirisha kwa kushindwa kumudu gharama za maisha, mahitaji kama vile kujipatia lishe ya uhakika, kugharamia elimu, matibabu kwa kaya husika na hata kutokuwa na makazi bora na ya uhakika, hivyo kukata tamaa na hivyo, kujikuta katika mazingira magumu kwa kushindwa kukidhi mahitaji yao ya msingi wakati wote.", "\u00a0", "Moja ya makazi ya mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.", "\u00a0", "Vikwazo vya ukuaji wa uchumi katika nchi masikini na zinazoendelea pamoja na sababu nyingine, vinaelezwa kuchagizwa kwa kiwango kikubwa na mfumo usiokuwa wa haki wa uendeshaji uchumi duniani.", "\u00a0", "Mataifa yaliyoendelea, hutumia fursa hiyo kuyanyonya yale masikini na hivyo kuathiri kwa kiwango kikubwa, mapambano dhidi ya umasikini kwa nchi masikini kama vile Tanzania.", "\u00a0", "Kwa kutambua tatizo hilo, serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii \u2013TASAF, imebuni Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (Productive Social Safety Net\u2013PSSN-), ambao moja ya malengo yake ni kuziwezesha kaya masikini zinazoishi katika hali duni.", "\u00a0", "Lengo mahsusi ni kuziwezesha kumudu \u00a0kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu, kama vile lishe, matibabu na elimu, ili kujenga rasilimali watu bora kwa manufaa ya taifa.", "\u00a0", "Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania\u2013 TASAF, unatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, \u00a0ambao ni wa aina yake kuwahi kutekelezwa nchini kwa njia ya kuhawilisha fedha kila mwezi, kwa kaya za walengwa wa mpango husika .", "\u00a0", "Takwimu za TASAF, zinazonyesha kuwa zaidi yaka ya kaya milioni moja nchini kote, zimetambuliwa na kuorodheshwa kwenye mpango huo na kiasi cha fedha, zaidi ya shilingi bilioni 95 zimetolewa kwa kaya za walengwa wa mpango nchini kote, tangu utaratibu huo ulipoanzishwa.", "\u00a0", "Ni utaratibu ulioanzishwa chini ya kivuli cha majaribio yaliyofanyika katika maeneo kadhaa ya utekelezaji nchini.", "\u00a0", "LENGO NA MAFANIKIO", "Tangu kuanza mpango huo, kumekuwapo mafanikio makubwa, hususan katika maeneo ya utambuzi, uandikishaji na hata uhawilishaji wa fedha (uhamishiaji fedha) kwa walengwa, ambao umefanyika kwa ufanisi mkubwa, ikilinganishwa na nchini nyingine, ambako utaratibu wa namna hiyo unatekelezwa.", "\u00a0", "Aidha, maisha ya walengwa yameanza kuonyesha mabadiliko makubwa hususan katika nyanja za elimu na matibabu kwa watoto wao mambo ambayo ni mojawapo ya masharti ya mpango, ikiaminika ni mahsusi kwa ajili ya kuijengea kaya uwezo kwa siku zijazo.", "\u00a0", "Mojawapo ya masharti ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, ni kwamba watoto wahudhurie masomo.", "\u00a0", "Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, pia umeweka mkazo mkubwa katika suala la kuboresha lishe ya walengwa, kwa kutambua kuwa lishe bora itawafanya wahusika kuwa na afya miongoni mwao, hususan kwa watoto na kuwasaidia katika makuzi yao kimwili na kiakili.", "\u00a0", "Hata hivyo, baadhi ya wananchi wamekuwa wakihoji namna walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wanavyopatikana.", "\u00a0", "Inahisiwa kuwa, ni hali inayotokana na mahitaji makubwa ya wananchi wanaotaka kujumuishwa kwenye mpango wenyewe.", "\u00a0", "TASAF imeweka utaratibu wa wazi wa namna ya kupata walengwa wa mpango huo wa kunusuru kaya masikini, ambapo wananchi kupitia mkutano mkuu wa vijiji husika, huorodhesha walengwa kwa kufuata vigezo vya umasikini, kulingana na mazingira ya eneo husika.", "\u00a0", "Vigezo hivyo, hutofautiana kutoka eneo moja hadi jingine. Hapo inajumuisha uduni wa makazi, uwezo mdogo wa kuhudumia kaya husika katika nyanja za elimu, afya.", "\u00a0", "Pia, kuna masuala kama uwezo wa kuanzisha miradi midogo huzingatiwa, ambapo baada ya taratibu zote kukamilika na kuingizwa kwenye mfumo maalumu, walengwa huanza kulipwa fedha kwa njia ya uhawilishaji fedha.", "\u00a0", "Baada ya kupata fedha kwa utaratibu wa uhawilishaji, idadi kubwa ya walengwa wameanza kuboresha maisha yao kwa kutumia sehemu ya fedha hizo, kuimarisha makazi yao kwa kuezeka nyumba zao kwa mabati, huku wengine wakitumia sehemu ya fedha hizo kuanzisha miradi midogo, ikiwamo ufugaji wa kuku, mbuzi, bata na kupanua shughuli za kilimo.", "\u00a0", "Katika kuhakikisha kuwa, kipato cha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kinaongezeka, Tasaf imeanzisha utaratibu wa kuwashirikisha walengwa wa mpango huo kuibua miradi na kuitekeleza kwenye maeneo yao kwa utaratibu wa ajira za muda.", "\u00a0", "Utekelezaji wake hufanywa kwa siku 15 za mwezi, ndani ya miezi minne kwa mwaka, wakati wa kipindi cha \u2018hari\u2019 na \u2018kasha\u2019 kulipwa fedha, baada ya kushiriki katika utekelezaji wa kazi husika.", "\u00a0", "Miradi inayoibuliwa na walengwa, ni ile ambayo jamii nzima katika kijiji au Shehia kwa upande wa Zanzibar, itanufaika nayo baada ya kukamilika ikiwamo uboreshaji wa mazingira, uchimbaji wa mitaro ya maji, hifadhi ya ardhi.", "\u00a0", "Ni utaratibu unaoonyesha mafanikio makubwa, tangu ulipoanza kutekelezwa kwenye maeneo mengi ya utekelezaji wa mpango husika.", "\u00a0", "Ni dhahiri, mpango huo wa kunusuru kaya masikini - PSSN, umeanzishwa \u00a0wakati muafaka, hasa ikizingatiwa kuwa idadi kubwa ya wananchi bado wanaishi katika hali ya umasikini.", "\u00a0", "Hivyo jitihada kama hizo zinapaswa kuungwa mkono na wadau mbalimbali wa maendeleo, huku walengwa wa mpango huo wakipaswa kuzingatia masharti yake na hatimaye waweze kuondokana na umaskini.", "\u00a0", "Mwandishi wa Makala hii ni msomaji wa gazeti la NIPASHE na anapatikana kwa simu namba: +255 754 266113", "\u00a0"], "byline": ["Na Waandishi wetu \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["TASAF yaibuka kunusuru familia na umasikini"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84215", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:56.826534"},
{"body": ["Kazi ni uhai. Huu ni msemo maarufu uliojaa ukweli mtupu. Ustawi wa mtu au jamii yoyote (likiwamo Taifa la Tanzania) hutegemea sana kwa kiasi gani, watu wake wanajituma kufanya kazi kwa bidii na maarifa, ili kuweza kujikimu na maisha pia kupata ziada ya akiba na uwekezaji katika maendeleo.", "\u00a0", "Ndiyo maana basi, dhana ya kazi imo hata katika katiba yetu ambamo katika sura ya haki za msingi na wajibu wa raia, suala la kazi limeainishwa bayana.\u00a0", "\u00a0", "Zaidi ya hapo, Katiba yetu ya mwaka 1977 inayotumika sasa inaeleza pia kwamba, yeyote yule anayefanya kazi anastahili kupewa ujira unaostahili kulingana na kile alichokifanya.\u00a0", "\u00a0", "Dhana hii imewahi kutiliwa mkazo pia na mahakama zetu hasa katika shauri muhimu la Butambala Dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania lililohukumiwa na hayati Jaji James Mwalusanya (kama alivyokuwa wakati ule).\u00a0", "\u00a0", "Zaidi ya hapo, Tanzania imesaini na kuridhia mikataba ya kimataifa ya ajira, inayozungumzia mambo haya na hivyo basi ni wajibu wa nchi kuiheshimu mikataba hiyo kama ilivyowahi kusisitizwa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania miaka kadhaa iliyopita katika shauri maarufu la Transport Equipment v. Valambhia.", "\u00a0", "Ile mtu atekeleze ipasavyo wajibu wake wa kufanya kazi pia kujipatia manufaa yatokanayo na hilo, yumkini basi ni lazima apatiwe yeye mwenyewe kuzitumia fursa zitakazomwezesha kufanya hivyo.", "\u00a0", "Hapo ndipo wajibu wa serikali unapojitokeza kwa uwekezaji wa mazingira mazuri yatakayomwezesha raia kufanya kazi kwa maslahi. \u00a0", "\u00a0", "Kwa hivyo basi, katika hili, serikali hutarajiwa kuandaa sera na pia kutunga sheria maridhawa zitakazotengeneza mazingira ya kukuza uchumi kwa kasi kunakoambatana na uongezwaji wa ajira mpya na pia kuimarisha zile zilizopo tayari.\u00a0", "\u00a0", "Basi katika, serikali inayowajibika katika kufanikisha jambo hili huimarisha sekta muhimu za kilimo na viwanda, kuboresha elimu katika ngazi zote, kuvutia wawekezaji wa ndani na nje, na pia kuandaa mfumo imara wa kifedha unaowawezesha watu kujipatia mitaji kupitia mabenki, masoko ya mitaji, kupunguza mifumuko ya bei ili kipato kinachopatikana kiwe na maana, na kadhalika.", "\u00a0", "Hata hivyo, ukiachana na kutazama iwapo ndiyo ama la Serikali imefanikiwa katika mambo hayo, serikali pia ina wajibu muhimu sana wa kuandaa sera, sheria \u00a0pia muundo wa kitaasisi mzuri kusimamia masuala ya mahusiano ya ajira, sambamba na mambo mtambuka kama vile utatuzi wa migogoro ihusiano na ajira, baina ya waajiri na waajiriwa, iwe katika ajira za umma ama katika sekta binafsi. Jambo hili ndilo mada yetu ya leo.\u00a0", "\u00a0", "Kwa hivyo basi, tujaribu basi kuzirejea sheria husika kuhusiana na mahusiano ya ajira, na hasa katika suala zima la usuluhishi wa migogoro hii ya kazi, pale mambo yanapoonekana kwenda kombo, baina ya mwajiri na mwajiriwa.\u00a0", "\u00a0", "Mada hii ya kisheria inahusiana sana na maendeleo ya kiuchumi kwa sababu kama mathalan mwajiriwa/mfanyakazi analipwa kiduchu, basi hata ari ya kufanya kazi pia ubunifu kazini vinapungua, na kwa ujumla uzalishaji ama huduma itolewayo na mfanyakazi huyu inakuwa chini ya kiwango na kuweza kuiathiri jamii nzima pia.", "\u00a0", "Kabla ya mwaka 2004, Tanzania ilikuwa na sheria tofauti tofauti za kazi, ingawa zilizokuwa muhimu zaidi zilikuwa ni Sheria ya Kazi iliyorithiwa kutoka Ukoloni (Employment Ordinance) pamoja na Sheria iliyohusika na Viwango vya Mishahara na Posho kwa Wafanyakazi pamoja na Kanuni kuhusiana na Masharti ya Mikataba ya Ajira (Regulations of Wages and Terms of Employment Act).\u00a0", "\u00a0", "Zaidi ya hapo, ni katika kipindi hicho ambacho nchi yetu chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere ikaonyesha nia ya dhati ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya kuonewa na waajiri wao, pale ilipotunga sheria muhimu sana iliyoitwa Security of Employment Act, 1964, miaka mitatu tu baada ya Uhuru wa Tanganyika, na pia mwaka ule ule ambao Muungano wetu uliasisiwa.\u00a0", "\u00a0", "Tumezizungumzia Sheria hizi ambazo hazitumiki tena tangu mwaka 2004 ili kujenga uelewa mpana zaidi kuhusiana na kule tulikotoka.\u00a0", "Prof. Issa Shivji ambaye pasipo shaka yoyote ndiye aliyefanya utafiti wa kina na kuandika machapisho muhimu kuhusiana na historia ya Sheria za Kazi za Tanzania, tangu ukoloni, amezizungumzia kwa undani sheria hizi na nyinginezo zinazohusika hapo.\u00a0", "Sambamba naye, machapisho mengine muhimu yaliyoandikwa na wataalam wengine mahiri wa sheria kama Dk.Wilbert Kapinga, Prof. Rutinwa na Dk. Tulia Ackson, wote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.", "\u00a0", "Mwaka 2004 Tanzania iliitunga Sheria mbili muhimu, ambazo ndizo zilizo muhimu zaidi, kwa vile ndizo zitumikazo katika mambo mengi muhimu ya kazi na ajira nchini mwetu.\u00a0", "Sheria ya kwanza ni Sheria namba 6 ya mwaka 2004 inayoitwa The Employment and Labour Relations Act, 2004 (Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi). Sheria ya pili ni Sheria namba 7 ya mwaka 2004 \u00a0inaitwa The Labour Institutions Act, 2004. Sheria hizi ziliandaliwa pamoja, miswada yake kupelekwa bungeni katika kikao kile kile na ikapitishwa kwa pamoja.\u00a0", "\u00a0", "Tofauti kubwa baina ya sheria hizi mbili ni kwamba ile ya Kwanza (namba 6) inahusika zaidi na mambo ya msingi kuhusiana na mikataba ya ajira pamoja na kutoa tafsiri \u00a0kuhusu nani ni mwajiri, nani mwajiriwa, aina za ajira zilizopo, sifa za mikataba ya ajira, haki na wajibu wa mfanyakazi na pia mwajiri, na kadhalika. \u00a0", "Ndani ya sheria hii kumeelezwa pia sababu ziwezazo kumfanya mtu aachishwe kazi, masharti ya muda wa kazi (pamoja na muda wa ziada), taratibu za likizo za kawaida, uzazi, mapumziko, usalama na ajali kazini, kuhamishwa kituo cha kazi, malipo ya kiinua mgongo na kadhalika.\u00a0", "\u00a0", "Kwa upande wake, Sheria namba 7 inahusika zaidi na haki na wajibu katika mahusiano ya kazi, kama vile kujiunga na vyama vya wafanyakazi, haki na taratibu za kugoma, miundo ya taasisi na pia mahakama zinazohusika na usuluhishaji wa migogoro ya kazi, pamoja na mambo mengineyo kama hayo.", "\u00a0", "Pamoja na mabadiliko yote hayo, Sheria zetu kwa kiasi fulani zimeweza luleta uwiano wenye kulenga kuimarisha uhusiano baina ya mwajiri na mwajiriwa \u00a0pia kuwapo mazingira ya upande mmoja kutojinufaisha dhidi ya mwingine. Ndiyo kusema, sheria na Mahakama hazitakubali kuona mwajiri akikatisha ajira au kumkata mshahara mwajiriwa bila kufuata misingi ya haki. \u00a0", "\u00a0", "Na ndivyo hivyo hivyo, sheria hizi hazilengi kumlinda mwajiriwa mzembe, mkorofi ama anayeshindwa kuwajibika kama mkataba wa ajira ulivyo ama matarajio ya mwajiri wake.\u00a0", "\u00a0", "Hukumu za Mahakama za Tanzania katika, mashauri kama Mahona v, University of Dar es Salaam; Simeon Manyaki v. Institute of Finance Management (IFM) na Obadiah Salehe v. Dodoma Wine Company (DOWICO) ni kielelezo dhahiri cha jambo hili.", "\u00a0", "Labda niseme tu, kwamba ingeleta mantiki zaidi katika safu hii leo kama tungejadili kwanza sheria namba 6 ya mwaka 2004 na kisha tukaizungumzia ile ya mahusiano ya ajira baadaye, lakini kwa sababu kadhaa wa kadhaa hili halikuweza kuwezekana.", "\u00a0", "\u00a0Hata hivyo, hili ni suala la mtiririko tu ambalo haliathiri chochote kuhusiana na yale yaliyomo ndani ya sheria hizo pamoja na uwezo wa msomaji wetu wapendwa kama wewe kushindwa kuelewa nini tunakizungumzia.", "\u00a0", "Kwa sababu sheria hii ya kazi ni ndefu ikiwa na sura zipatazo 65 na taratibu nyingi katika masuala ya mahusiano ya ajira, taasisi za utatuzi wa ajira, masharti ya migomo na kadhalika leo ninaishia hapa.", "\u00a0", "*Denis Maringo ni Mwanasheria aliyeko Dar es Salaam. Anapatikana kwa simu namba 0719270067. Barua-pepe: dnmaringo@gmail.com", "\u00a0"], "byline": ["Na Waandishi wetu \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Sheria za Ajira na Mahusiano ya Kazi"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84217", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:57.461201"},
{"body": ["Kuna ukweli kwamba uchaguzi ndiyo mwarobaini wa majigambo ya wanasiasa. Ukitaka kujua ukweli wa jambo hili, jaribu kuhudhuria mihadhara ya mikutano ya kampeni za siasa. Sitanii utakuta mzee wa miaka 60 anampa shikamoo kijana wa miaka 20, ilihali ni kutafuta ushindi .", "\u00a0", "Sambamba na hilo, ikifika kipindi cha uchaguzi utawaona \u00a0wagombea wakimwaga sera mithili ya mitume \u00a0wa Yesu walioandikwa kwenye Biblia Takatifu. Kipindi kama hicho utasikia ahadi kemkem kama vile kuleta mabadiliko au mageuzi ya kisiasa katika taifa.", "\u00a0", "Sipingani na dhana hii ya kuchagua viongozi kwasababu ndiyo taratibu kuu ya kufikia kwenye demokrasia ya kweli. Tumeanza kusikia majigambo ya wanasiasa kutoka vyama mbalimbali wakija na kauli mbiu \u00a0kama vile \u201cmabadiliko ni lazima\u201d.", "\u00a0", "Ukifuatilia hotuba za wagombea urais hususani kutoka vyama hivi viwili hasimu chama tawala (CCM) na Chadema kinachowakilishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi \u00a0(Ukawa). Kusema ukweli kila mgombea anajaribu kwa kadiri anavyoweza kuwaaminisha Watanzania kuwa chama chake ndicho kina uwezo wa kuleta mabadiliko chanya na ya kweli.", "\u00a0", "Itakumbukwa kuwa baada ya harakati za kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 1961 na ule wa Zanzibar kupitia Mapinduzi ya Januari 12, \u00a01964 TANU na ASP, ziliendelea kukabiliwa na majukumu ya kuendeleza mapambano ya ukombozi katika Afrika na kuimarisha umoja na mshikamano wa kimataifa.", "\u00a0", "Aidha, katika kipindi hicho Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alitoa changamoto akiwataka viongozi wenzake na wanachama wajitayarishe kupokea mabadiliko ambayo yalikuwa hayana budi kufanyika. Shabaha kuu ilikuwa ni kulitoa taifa katika hali ya unyonge, kiuchumi na kulifikisha katika hali ya ustawi na maendeleo pevu. Hivyo ikaanzishwa Azimio la Arusha.", "\u00a0", "Nukuu muhimu katika ukurasa wa tisa wa kitabu cha Azimio la Arusha inatamkwa haya:-", "\u201cTumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyanyaswa kiasi cha kutosha na tumepuuzwa vikali . Unyonge wetu ndiyo uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi, mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na wala tusipuuzwe tena.\u201d", "\u00a0", "Ninachotaka wasomaji wakielewe ni kwamba majigambo ya wanasiasa katika kuleta mapinduzi ya kuindoa nchi kwenye unyonge wa kiuchumi haujaanza hivi leo.\u00a0", "\u00a0", "Ndiyo maana ninaposikia hotuba ya mgombea wa CCM \u00a0Dk. John Magufuli naanza kupata \u00a0matumaini kwamba huenda Tanzania ikampata Rais wa uhakika ambaye ataleta mabadiliko ya kweli kama alivyowahi kusema Mwalimu Nyerere.", "\u00a0", "Katika kitabu cha Azimio la Arusha Nyerere anasema \u201cTumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyanyaswa kiasi cha kutosha !.... Mgombea wa \u00a0CCM \u00a0Dk. Magufuli hakupenda kuficha ukweli kwenye hotuba zake kwamba jamii imeonewa vya kutosha na kunyanyaswa vya kutosha katika kutafuta haki ya kupata maisha bora kwenye nchi yao.", "Hotuba ya Dk. Magufuli siku ya ufunguzi jijini Dar es salaam na ile ya Morogoro, ilinigusa na nikahisi kwamba huenda kwa sasa Watanzania watampata rais anayetambua wananchi wanataka mapinduzi ya \u00a0kuondoa unyonge ili wasionewe wala kupuuzwa tena.", "\u00a0", "Kwenye baadhi ya hotuba zake mgombea huyu \u00a0amenukuliwa akisema; \u201cAnatambua kuwa wananchi wanahitaji mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko\u201d. Ukisikiliza hotuba zake kwa makini hakika utatambua kwamba anatamka kutoka kwenye sakafu ya moyo wake.", "\u00a0", "Anasema \u201cmimi ni kazi tu\u201d na kwamba yeye siyo mwanasiasa bali ni mtendaji. Dhamira yake ndiyo imenifanya nirejee historia ya utawala wa Mwalimu Nyerere ambaye aliamua kuanzisha Azimio la Arusha ili kuleta mapinduzi ya usawa.\u00a0", "\u00a0", "Mkabala huu wa kihistoria wa kutafakari chimbuko la siasa ya nchi yetu na mkondo wa harakati za ukombozi ndio umenisukuma kumwamini Dk. Magufuli kwamba anachokihubiri majukwaani hakika yanatoka kwenye sakafu ya moyo wake. Nayaona mabadiliko ya kweli .", "\u00a0", "Mgombea huyu \u00a0alinukuliwa akisema. Siyo lazima eti wananchi wakitaka mabadiliko basi shurti wabadilishe uongozi uliokuwepo \u00a0akimaanisha chama tawala.\u00a0", "\u00a0", "Ifahamike kwamba, tendo la kufanya majaribio mara nyingi huishia kwa kusema \u201cmajuto ni mjukuu\u201d. Inatubidi tutafakari kwa undani kabla ya kufikia maamuzi yanayoweza kutuondolea amani na mshikamano.", "\u00a0", "Wahenga walisema \u201cfimbo iliyo mbali haiui nyoka\u201d Dk. Magufuli anaonekana kama ni mtu aliyetengenezewa njia kama alivyokuwa Yohana Mbatizaji. Hakuna aliyetegemea Magufuli angefika hapo alikofikia.\u00a0", "\u00a0", "Maajabu ya Mungu ni mengi. Hatujui kama mgombea huyu \u00a0alitengenezewa njia ya kufikia urais na Mungu. Hebu tujiulize? Iweje mtu atoke na kikoba chake halafu achukue fomu na kukirudisha bila kusindikizwa hata na mpambe mmoja na kweli akaupata! Jibu laweza kuwa ni kwamba Mwenyezi Mungu anatumia watu wake kimya kimya katika kutaka kutekeleza mabadiliko ya kweli duniani.", "\u00a0", "Hivyo haishangazi kama hilo nalo huenda ni mkono wa Mungu. Ndiyo maana nasema \u201cNayaona mabadiliko mbele yetu kama enzi za Nyerere.", "J. M. Kibasso", "Simu; 0713-399004/0767-399004", "Email:jmkibasso@gmail.com"], "byline": ["Na John Kibasso\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Yapo mabadiliko hotuba za Magufuli kama ilivyokuwa kwa Nyerere."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84245", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:57.853911"},
{"body": ["Baada ya msimu wa kula na kuliwa, kugeuzana majuha, kuuzana, kutalikiana, kusalitiana hata kumalizana kufunguliwa, kila msanii amejiandaa na sanaa zake kuhakikisha anachuma.", "\u00a0", "Hapa walevi ndiyo walengwa wakubwa wakiwamo mafisi na mafisadi na wanasiasa wenye mshiko waliouchapa kwa walevi. Kila msanii anataka apige tena hela ndefu aondoke na chake.", "\u00a0", "Juzi mzee mwenyewe ilibidi nipige bangi na kanywaji kama sina akili nzuri baada ya kumuona msanii mmoja akitangaza eti ana mpango wa kuendesha sala na matamasha ya kuombea uchakachuaji!", "\u00a0", "\u00a0Kwa vile ni rahisi kuwaliza wadanganyika, napanga kuandaa tamasha na mikesha ya kuombea hotuba ya mgombea mpendwa ipendwe na nambari wahedi waendelee kuwa kwenye ulaji hata kama hawafai. Ili kuwaingiza kisawa sawa nina mpango wa kuombea hata magari na vipaaza sauti, \u00a0hoteli psmoja na viwanja watakavyotumia \u00a0wagombea wapendwa wa chama pendwa viwe salama.\u00a0", "\u00a0", "Nitaandaa mkesha na matamasha mengine ya kuomba wapingaji washindwe, kukakamaa na kunyong\u2019onyea.", "Funga kazi ni hii , nitaandaa mikesha na matamasha ya kuhamasisha wazazi wawalazimishe watoto wao kupigia kura chama pendwa. Wasipofanya hivyo wawaachie laana kali ikibidi iwe sawa na ya kulaani jua ligeuke jiwe!", "\u00a0Pia katika mikesha hii nitaombea ndata wafanikiwe kutoa vitisho kwa wapingaji wasiseme baadhi ya mambo wakashtakiwa.\u00a0", "\u00a0", "Unajifanya unaombea uchakachuaji, amani maendeleo na mengine wakati ukishuhudia siasa za shari, ujambazi, ufisadi na jinai. Kama tutakuwa wakweli, hapa amani itapatikana wapi bila haki? Maendeleo yatapatinaje bila uwajibikaji na uchapakazi?", "\u00a0", "\u00a0Hata tungeomba miaka 1,000,000 na kukesha uchi, Mungu ni wa haki. Hatatoa hizo baraka na vyote tunavyoongopa kuwa tunaombea. Jisaidie nikusaidie. Ukipanda mbigiri usitegemee kuvuna maua aina ya uwaridi au jasmin. Ukichagua ufisadi utegemee ufisadi. Ukipenda mabadiliko utegemee mabadiliko. Simple", "\u00a0Hebu tuwe serious kidogo. Hivi lipi la maana, kumwambia mwanao akapige kura au akadai haki? Hawa wachovu wa kiakili wanaokuja na usanii kama huu kwa vile usanii umewashinda sasa wanataka siasa kweli ni wabunifu au wana ndoto za kubuni? Tusiombee uchakachuaji.\u00a0", "\u00a0", "Badala yake tupiganie haki. Tulaani ufisadi, uzembe, usanii, ushenzi na upuuzi wa kila aina kama kila mtu kujifanya anaipenda kaya wakati anaihujumu. Hivi hawa wavivu wa kufikiri wanaowekeza katika kuomba badala ya kuamba ukweli wana maana kweli? Tumekuwa kaya ya wasanii watupu!", "\u00a0", "\u00a0Nilimuona yule binti aitwaye Ubaya (the opposite) Koleo aliyekataa kuleleka akijinadi kuwa anawahamasisha akina mama wawambie watoto wao wakapige kura. Well, mbona ameanzisha ubaguzi? Kwanini asiwaombe wazazi wote wawili badala yake awaombe wanawake? Usitake kutubagua na mamisahib wetu.", "\u00a0", "\u00a0 Ngoja niongee kama kidhabu huyu wa kike apendaye kuchanganya kikameruni ka kiswa akitaka aonekane amebukua wakati hovyo. \u00a0By the way, why are you openly discriminating againt the opposition? My understanding is that you are supposed to be neutral as an artist. Njaa nyingine bwana!", "\u00a0", "\u00a0Sitashangaa kusikia kesho wajalaana fulani wenye njaa kama fisi wakiandaa kila aina ya upuuzi kuunga mkono upuuzi na jinai nyingine. Kaya yetu inahitaji kuombewa bali kuambiwa ukweli kuwa inanuka ufisadi na kutawaliwa na wasanii, wachovu na mafisadi wanaopaswa kufungashiwa virago wakaenda kumalizi maisha lupango.\u00a0", "\u00a0", "Kama mnaipenda kaya na si kuiponda kwanini msiwaombee walevi wazinduke na kuwatimua watesi wao? Haya masuala ya kuomba washitiri wenu wasifumaniwe au kutimuliwa kwenye ulaji yanaboa kuchosha na kukera", "\u00a0Wahenga walijisemea: Wajinga ndiyo waliwao. Acha nifafanue isomeke Wadaganyika ndiyo wadanganywao.\u00a0"], "byline": ["Na Nkwazi Mhango, canada\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Walevi mjipange mmewaona wajanja"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84243", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:58.503812"},
{"body": ["Msimu wa 2015/16 wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ulianza rasmi juzi ukishirikisha timu 16, mbili zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita.", "\u00a0", "Tayari wadhamini wakuu wa ligi hiyo, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wameshakabidhi vifaa kwa timu zote shiriki huku wakiongeza kipindi kingine cha miaka mitatu kuendelea kuidhamini ligi hiyo kubwa zaidi nchini.", "\u00a0", "Mbali na neema hiyo ya udhamini wa Sh. bilioni 6.7, kampuni hiyo pia itaendelea kutoa zawadi ya Sh milioni moja ya Mchezaji Bora wa kila mwezi, utaratibu ambao iliuanzisha msimu uliopita. Tukiwa wadau namba moja wa michezo nchini, Nipashe tunawapongeza Vodacom kwa kuendelea kudhamini ligi hiyo na kutoa zawadi kwa wachezaji waaong\u2019ara kila mwezi na msimu mzima.", "\u00a0", "Hata hivyo, tunatoa rai kwa wasimamizi wakuu wa ligi hiyo, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ambayo ni moja ya vyombo vya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuhakisha kunakuwa na utaratibu bora na sahihi wa kuwapata washindi wa zawadi husika. Tunaukumhusha uongozi mpya wa TFF kwamba sehemu kubwa ya zawadi za Mchezaji Bora wa Mwezi msimu uliopita zilikwenda kwa watu wasio sahihi kutokana na kile ambacho tunaamini kutozingatiwa kwa taratibu sahihi za kumpata mshindi wa tuzo hiyo.", "\u00a0", "Kwa kuzingatia kwamba shirikisho lina upungufu wa wataalam wa takwimu, tunaishauri uigwe utaratibu unaofanywa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kuwaachia wataalam wa vituo vya televisheni vinavyoingia ubia wa kudhamini mashindano, wachague Mchezaji Bora wa Mwezi.", "\u00a0", "Kampuni ya Azam Media ndiyo imenunua matangazo ya televisheni ya Ligi ya Bara. Ni vyema kampuni hiyo ikapewa jukumu la kuteua Mchezaji Bora wa Mwezi na baadaye Mchezaji Bora wa Ligi badala ya jukumu hilo kuachwa kwa jopo la makocha la TFF ambalo msimu uliopita lilionyesha udhaifu katika kuwapata washindi sahihi wa tuzo mbalimbali za ligi hiyo.", "\u00a0", "Miezi miwili iliyopita moja ya kampuni zinazojihusisha na matangazo ya moja kwa moja ya michezo ilinunua haki za matangazo ya michuano ya Kombe la Kagame jijni Dar es Salaam na ndiyo iliyopewa jukumu la kuchagua Mchezaji Bora wa kila mechi na baadaye Kipa Bora, Beki Bora, Mfungaji Bora na Mchezaji Bora wa mashindano.", "\u00a0", "Kutokana na kuwa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kutunza kumbukumbu za mechi zote za Kombe la Kagame mwaka huu, kampuni hiyo ilitangaza Mchezaji Bora wa kila mechi na michuano kwa ujumla na hapakuwa na malalamiko dhidi ya waliotangazwa washindi, tofauti na ilivyokuwa kwa tuzo za wateule wa TFF katika msimu uliopita wa Ligi ya Bara.", "\u00a0", "Nipashe tunaamini Azam TV watatupatia washindi sahihi wa tuzo za ligi hiyo msimu huu ikiwa watapewa jukumu hilo na TFF kutokana na vifaa vya kisasa (vya mfumo wa HD) ambavyo wameanza kuvitumia msimu huu.", "\u00a0", "Tunalishauri shirikisho liachane na utaratibu wa msimu uliopita wa kuteua makocha kutoka \u2018Jopo la Makocha la TFF\u2019 kwenda kutazama mechi na kisha kutupatia Mchezaji Bora wa Mwezi kwa vile msimu uliopita utaratibu huo haukuwa na matokeo chanya. Shime, TFF inapaswa kuhakikisha kunakuwa na taratibu sahihi za kuwapata washindi wa tuzo za Ligi Kuu ili kuwatendea haki wadhamini wa ligi hiyo na soka la Tanzania kwa ujumla.", "\u00a0"], "byline": ["Na Editor \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Tuzo ligi Kuu Bara zisimamiwe vizuri."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84282", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:59.507128"},
{"body": ["Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, imekamata pombe mbalimbali bandia za \u2018viroba\u2019 aina ya rider, empire, na signature vodka, zilizokuwa zikidaiwa kutengenezwa bila kibali na kiwanda cha Mwanza Lakeline Ltd, zikiwa zimehifadhiwa ghala la kampuni ya Ikohi lililopo jijini Mwanza.", "\u00a0", "Bidhaa hizo ziligunduliwa katika ukaguzi wa kushtukiza uliofanywa na mamlaka hiyo zikidaiwa kuhifadhiwa katika ghala hilo linalomilikiwa na kampuni ya Ikohi, lakini zikidaiwa zilitoroshwa katika kiwanda cha Mwanza Lake Line, wakati kikifanyiwa ukaguzi na mamlaka hiyo.", "\u00a0", "Akizungumza na NIPASHE juzi, Mkaguzi wa TFDA Kanda ya Ziwa, Nuru Mwasulama, alisema kiwanda hicho kilichopo jijini Mwanza, hakijasajiliwa kuzalisha bidhaa hizo zilizokamatwa, hivyo kilikuwa kikizalisha kwa njia ya ujanja wakati \u2018viroba\u2019 vya kuwekea pombe hiyo vikinunuliwa nchini Uganda.", "\u00a0", "\u201cTumechukua hatua ya haraka kukifungia kiwanda hicho na kuzuia bidhaa zake kutokana na kucheza mchezo mchafu na kuhatarisha afya za watumiaji wa bidhaa hizo,\u201d alisema Mwasulama.", "\u00a0", "Alisema baada ya kufanya msako wa kushtukiza kiwandani hapo, siku ya kwanza hawakufanikiwa kuingia ndani, lakini waliona \u2018mzigo\u2019 ukiwa ndani ya kiwanda kupitia dirishani, isipokuwa kilichofanyika ni mmiliki wa ghala la Ikohi kuuhamisha usiku na kuuweka ghalani mwake ili usambazwe kwa walaji bila ya ruhusa ya mamlaka.\u00a0", "Mwasulama alisema kiwanda hicho kilipewa kibali na mamlaka kusindika pombe ya \u2018viroba\u2019 aina ya simba gine pekee, lakini walikiuka masharti ya leseni na kuzalisha bidhaa ambazo hawakupewa kibali kuzalisha.", "\u00a0", "Alisema bidhaa zilizokamatwa ni masanduku 1,246 na magunia 25, ambayo thamani yake inakadiriwa kuwa Sh. milioni 75.", "\u00a0", "Hata hivyo, mmiliki wa ghala hilo, Ikohi alikataa kuzungumza na waandishi wa habari kwa madai msemaji ni mmiliki wa kiwanda cha Mwanza Lakeline, Chola Maginga, ambaye yupo safarini China."], "byline": ["Na Waandishi wetu \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["TFDA yakamata bidhaa 'feki' iliyotoroshwa."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84302", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:59.514037"},
{"body": ["Korosho ni moja ya mazao makuu ya biashara nchini, ambalo limekuwa likisafirishwa nje ya nchi kama malighafi \u00a0hivyo kuikosesha nchi faida nyingi ambazo zingepatikana kama zao hilo lingeongezewa \u00a0thamani kwa kuuzwa zikiwa zimebanguliwa.\u00a0", "\u00a0", "Zao hilo, hulimwa kwa wingi \u00a0katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania, yaani Lindi na Mtwara ikifuatiwa na Ruvuma, Pwani na Tanga.", "\u00a0", "Wakulima wengi wa zao hilo, kwa miaka mingi wamekuwa wakilalamikia kuhusu mazingira duni ya hifadhi na vifaa vya kubangulia korosho, hususan kwa wakulima wadogo wadogo.", "\u00a0", "Serikali ilipokuwa ikitekeleza sera ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma, ilivikumba pia viwanda 12 vya kubangua korosho nchini. Tangu hatua hiyo ichukuliwe, mwenendo wa uzalishaji na ubanguaji wa korosho nchini umekua wa kubahatisha zaidi. Viwanda hivyo baada ya kubinafsishwa ni kama vimegeuzwa maghala ya kuhifadhia mazao.", "\u00a0", "Ubanguaji wa korosho, miongonni mwa faida zinazopatikana kwa ubanguaji wa zao hilo ni kutengeneza ajira za watu viwandani hasa wanawake, bidhaa zitokanazo na ganda la korosho, kupanua wigo wa soko la zao hilo ikilinganishwa na soko la korosho lililopo nchini India.\u00a0", "\u00a0", "Kwa upande wake, Jukwaa Huru la Wadau wa Sekta ya Kilimo nchini (Ansaf) kwa kushirikana na Serikali, imeendelea kujenga mazingira ya kuwawezesha wabanguaji wa korosho nchini kabla ya zao hilo kusafirishwa nje ya nchi. Miongoni mwa mikakati hiyo ni \u00a0kutoa elimu bora ya ubanguaji korosho.\u00a0", "\u00a0", "Kauli ya Wakulima\u00a0", "Mwidini Bakari, mkulima wa korosho wilayani Newala anasema kuwa wana vikundi 21 vya ubanguaji korosho vyenye wakulima 448. Hata hivyo, wanakabiliwa na tatizo la kushindwa kufikia \u00a0kupata korosho safi kutokana na kutumia zana duni.", "\u00a0", "Kazi ya kubangua korosho anasema kuwa, inahitaji mashine za kubangua na meza zake, mashine ya kuoka na kukaushia, vyombo vya kutunzia korosho, meza za kupangia madaraja na mashine ya kufunga.\u00a0", "\u00a0", "Pia anasema kuna \u00a0changamoto ya kukosekana kwa maeneo maalumu ya kufanyia shughuli za ubanguaji kwa vikundi vidogo hivyo ni vigumu kutambulika pamoja na \u00a0kupata masoko ya korosho zilizobanguliwa.", "\u00a0", "Katibu wa wabanguaji korosho wadogowadogo wilayani Tandahimba, Said Kawa anasema kuwa wana vikundi vidogovidogo 23 vya kubangua korosho, lakini hadi sasa hawajapata soko la uhakika la kuuzia korosho zao.", "\u00a0", "\u201c Hadi sasa tunauza korosho kama wamachinga.Tunajitwisha kichwani tunatembeza mtaani, hadi sasa hatujapata soko la uhakika na tumehangaika bila ya mafanikio yoyote,\u201d anasema Kawa.", "\u00a0", "Mwaka jana anasema kuwa, walizalisha tani 58,000 za korosho wilayani humo, lakini wameshindwa kuziuza kutokana na kukosa ubora uliosababishwa na kubanguliwa vibaya.", "\u00a0", "Anasema mbanguaji mdogo wa korosho anapoifanya kazi hiyo katika mazingira safi, salama na kwa ubora, husaidia upatikanaji wa soko la uhakika ndani na nje ya nchi.", "\u00a0", "Katika hatua nyingine, wabanguaji wengi wadogo wamejikuta wanashindwa kuwa na miradi endelevu kwa sababu ya kukosa elimu ya kusimamia fedha, ubora, masoko na rasilimali watu.", "\u00a0", "Ali Msanjo, mkulima wa korosho wilaya ya Tunduru anasema \u00a0kuwa wana vikundi 22 vya kubangua korosho \u00a0vilivyosajiliwa.", "\u00a0", "Anasema wanakabiliwa na changamoto lukuki zikiwamo, ukosekanaji wa masoko, kutokuwa na vifaa vya ubanguaji, mitaji, vifungashio.", "\u00a0", "Naye Kudra Msumi, mkulima wa korosho kutoka Mkuranga mkoa wa Pwani anasema kuwa, wao wana vikundi 12 vya kubangua korosho, na wanachama 202.", "\u00a0", "Anasema, wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa pembejeo, dawa kwa ajili ya kupulizia korosho, ukosekanaji wa mitaji, ufahamu mdogo kuhusu zao la korosho unaochangia kupatikana mavuno machache, pamoja na sera ya stakabadhi gharani kuwakandamiza wakulima.", "\u00a0", "Tumpale Maghelema, kutoka wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi, ambaye pia ni mratibu wa wabanguaji wadogowadogo wa korosho anasema kuwa, wana umoja wa wabanguaji korosho Ruangwa uitwao Wakoru.", "\u00a0", "Mwaka 2010 wanasema \u00a0walikuwa na vikundi 12, lakini mwaka huu wanavikundi 23, kati yao \u00a0wanawake ni 169 wanaume ni 97. Kila mwanachama anabangua kilo 30 hadi 40 za korosho kwa siku.", "\u00a0", "Kuhusu \u00a0changamoto wanazokabiliana nazo anasema \u00a0ni kutokuwapo majengo ya kufanyia kazi ya kubangua korosho, hivyo kuwafanya wabangue korosho katika mazingira magumu.", "\u00a0", "\u201c Tunabangulia korosho nje\u2026 mvua ikinyesha \u00a0au hali ya hewa ikibadilika ghafla, basi nasi tunasimamisha shughuli zetu,\u201d anasema.", "\u00a0", "Changamoto nyingine anazitaja kuwa ni pamoja na kutokuwa na vifungashio vya korosho, malighafi, ukosefu wa elimu ya kubangulia korosho, ukosefu wa \u00a0umeme wa kukaushia korosho hivyo kuwafanya watumie moto wa mkaa kukaushia korosho.", "\u00a0", "Swalehe Ntwale, kutoka kijiji cha Nanyumbu wilaya ya Masasi \u00a0ambaye pia ni katibu wa wabanguaji wadogowadogo wa korosho anasema kuwa wanavikundi sita za kubangua korosho.", "\u00a0", "Miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na bei ndogo ya korosho Sh. 1,200 kwa kilo moja, inayowarudisha nyuma kimaendeleo kwa kushindwa kupata faida, ukosefu wa majengo ya kubangulia korosho pamoja na elimu ndogo ya kilimo cha zao hilo.", "\u00a0", "\u201cKwa mfano kupata vifungashio ni shida, hadi twende Dar es Salaam, mauzo shida, soko la kuuzia korosho siyo la uhakika, vifaa vya kubangulia hatuna tunatumia nyundo, mitaji midogo,\u201d anasema Ntwale.", "\u00a0", "Marina Bakari, mbanguaji wa korosho wa kujitegemea kutoka wilayani Tandahimba mkoani Mtwara, anaeleza kuwa kutokuwa na vifaa vya kisasa vya kubangulia korosho inamlazimu kutumia chuma kubangulia korosho.", "\u00a0", "Katika mazingira hayo, anasema \u00a0akishamaliza kubangua korosho, hujitwisha kichwani ili \u00a0kutembeza mtaani, na humchukua muda wa mwezi mzima kumaliza korosho zilizojaa kwenye ndoo ndogo ya lita tano.", "\u00a0", "Hufungasha korosho kwa kutumia mshumaa. Kilo moja ya korosho huuza kati ya Sh. 9,000 hadi 8,000. Kwa fungu huuza Sh. 500.", "\u00a0", "Naye Zena Kihangu kutoka Nachingwea anaeleza kuwa, mwaka 2007 waliunda vikundi vidogovidogo vya ubanguaji wa korosho 30 baada ya kuona soko la korosho linayumba wilayani humo.", "\u00a0", "Ukosefu wa vitendea kazi, ukosefu wa elimu ya ubanguaji korosho, ukosefu wa masoko anasema kuwa ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wilayani humo.", "\u00a0", "Kauli ya Bodi ya Korosho", "Meneja ubanguaji wa \u00a0Bodi ya Korosho nchini (CBT), Shabani Yahaya Simuli anakiri kuwapo matatizo yanayowakabili wakulima wa korosho hususan wabanguaji wadogowadogo.", "\u00a0", "Anabainisha matatizo hayo ni kama vile, kutokuwapo vitendea kazi, vifungashio, \u00a0masoko ya uhakika na \u00a0ukosefu wa elimu ya ujasiriamali.", "\u00a0", "Anasema CBT wanatilia mkazo utoaji elimu kwa wabanguaji hao, kwani wanafahamu inaongeza ajira na kwamba hadi sasa wamevifikia vikundi 232 vya ubanguaji.", "\u00a0", "Uamuzi wa \u00a0serikali kuviuza viwanda 12 vya kubangulia korosho anasema kuwa, umechangia kwa asilimia kadhaa kuwapo matatizo kwa wabanguaji wadogowadogo wa korosho.", "\u00a0", "Anasema kwa sasa Tanzania iko nyuma katika ubanguaji wa korosho. Takwimu za mwaka jana kati ya tani 200,000 za korosho zilizozalishwa ni tani 20,000 tu zilibanguliwa.", "\u00a0", "\u201cTatizo la utozaji kodi kwa vifaa vitumikavyo katika ubanguaji, vifaa vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi, vinatozwa kodi hivyo kusababisha kupanda gharama za uzalishaji na kufanya korosho zinazozalishwa kuwa ghali katika soko la dunia,\u201d anasema.\u00a0", "\u00a0", "Vifaa hivyo ni pamoja na vifungashio vinavyotumika na mashine za kisasa za ufungaji na maboksi ya kufungashia na mzigo wa kodi.", "\u00a0", "Changamoto nyingine zinazoikabili bodi hiyo ni ugumu wa upatikanaji wa soko la uhakika la korosho zinazobanguliwa nchini kutokana na ushindani uliopo katika masoko.\u00a0", "\u00a0"], "byline": ["Na Waandishi wetu \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Zana duni kizingiti kwa wabangua korosho kukuza uchumi"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84211", "scraped_at": "2015-09-14T11:43:59.860535"},
{"body": ["Wiki hii Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ameibuka ndani ya vyombo vya habari \u2018kumpopoa\u2019 Katibu Mkuu wa Chadema, aliyejiondoa kwenye siasa kwa madai ya kupinga ujio wa Edward Lowassa ndani ya chama hicho. Hata hivyo Askofu Gwajima anampinga kuwa kilichomuondoa Chadema ni kupingwa na mchumba wake, aliyetaka awe rais naye apewe heshima ya mama wa Ikulu .", "Kiongozi huyo wa kiroho, ameibua mambo mengi ambayo wapo wanaounga mkono hatua hiyo lakini kuna baadhi wanaoitafsiri kwa kuipa sura ya kidunia na si kiroho maana pengine kama kiongozi wa imani asingefanya hivyo. Pamoja na hisia hizo viongozi wenzake wa kiroho wanasema kutoka kwa \u2018waraka wa Gwajima\u2019 kuna cha kujifunza kama anavyoeleza Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste, William Mwamalanga. (Pichani).", "\u00a0", "Mchungaji huyu anazungumza na Nipashe na kugusia baadhi ya mambo ya kukwepa ili kuepusha athari zaidi.", "\u00a0", "KUKASHIFU KANISA", "Kama kiongozi wa kanisa anaelezea kukerwa na baadhi ya wanasiasa wanaosukuma tuhuma kwa viongozi wa dini wakiwahusisha na rushwa.", "\u00a0", "Mathalani kudai kuwa maaskofu wamehongwa kati ya Shilingi milioni 60 hadi 300 ili kumkubali mgombea mmojawapo, ni mambo yanayowafanya waumini kuwafikiria vibaya viongozi wao.", "\u00a0", "Anasema mbali na rushwa wapo baadhi ya wagombea na hata viongozi ndani ya jamii wanaohubiri siasa za chuki kuwa baadhi ya makabila ya Tanzania hawafai kuwa rais wa nchi hii.Kadhalika anasikitishwa na wagombea wanaodai kuwa upinzani unasababisha uvunjifu wa amani na hata kutumia mifano ya machafuko katika baadhi ya nchi za Afrika kuwa ziliamua kuua viongozi wao na sasa raia hao wanahangaika.", "\u00a0", "Anawataka Watanzania kufahamu kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi. \u201cNataka kusisitiza kwa wanasiasa na Watanzania kwa ujumla wetu kuwa yapo maisha kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.", "\u00a0", "\u201cIli amani yetu iendelee ni lazima tuache uongo, udini, utaifa wa kujibagua kwa mfano \u2018ubara au uzanzibari\u2019 hata ukanda kwani hiyo ndiyo mitaji ya kuangamiza taifa na wala siyo kuwa na wanachama wa upinzani.\u201d", "\u00a0", "Anasema upinzani ni jicho la ziada la kukosoana na upo kikatiba na si mtaji wa kuvunja amani kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa. \u201cNawashauri wanasiasa kuwa upendo, amani , haki na wajibu wa kila mtu katika kutunza umoja ziwe kauli zenu.\u201d", "\u00a0", "\u2018UONGO NI MATUSI\u2019", "Askofu Mwamalanga akizungumzia madai ya kuzuliana kama kupewa hongo na kusingiziana anasema kauli za uongo hazina tofauti na hotuba za matusi au kukashifu kwani zinahamasisha hasira ndani ya jamii hivyo kuwa chanzo cha vurugu na kuzalisha mitandao ya uovu jambo ambalo ni hatari kwa vile linatoa mwanya kwa maadui wa ndani na nje kujipenyeza na kuhatarisha umoja na amani ya nchi.", "\u00a0", "UVUMILIVU WA LOWASSA", "Askofu Mwamalanga anamtaja mgombea wa urais kupitia umoja wa vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD Edward Lowassa, kuwa mfano wa uvumilivu wa kuigwa kwani pamoja na kuporomoshewa matusi, kulaumiwa na watu wengi kwenye kampeni amekuwa mtulivu na mwenye kulenga ujumbe anaotaka kuuwasilisha kwa wapiga kura.", "\u00a0", "Badala ya kutumia majukwaa kujibu matusi Lowassa amekuwa mtulivu na kutaka wale wenye ushahidi wauwasilishe, hivyo wanasiasa wengine wajifunze na huo ndiyo ustarabu wa kisiasa.", "\u00a0", "\u201cNawaomba wanasiasa muigeni Lowassa anafahamu kuwa kuna maisha kabla na baada ya uchaguzi.\u201d", "\u201cNapendekeza baada ya uchaguzi mkuu itolewe tunzo ya utulivu au heshima wakati wa kampeni. Naamini kwamba hii itasaidia wagombea na wapambe wao kuwa watulivu wakati wote wa kampeni na baada ya uchaguzi Mkuu ili kulinda amani na utlivu wa nchi.\u201d", "\u00a0", "VYOMBO VYA ULINZI", "Anapozungumzia \u2018jeuri\u2019 ya Dk Wilbroad Slaa, kuwa analindwa na maofisa wa usalama wa taifa, anaona kuwa si jambo la kutamba kwa vile linatoa nafasi kwa watu kuwaza na hata kuzua mambo mengine ambayo hayaleti amani.", "Anasema vyombo vya umma kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na majeshi mengine yalinde umma siyo mtu binafsi.", "\u00a0", "Vyombo hivi ni muhimu \u00a0katika kusimamia haki na kuendelea kuwakumbusha wanasiasa na Watanzania kuhusu uchaguzi huku vikibeba jukumu la kuufanya umma uwe wa utulivu na amani kwa ustawi wa taifa.", "\u00a0", "Anaamini kiongozi wa siasa kutukana na kutoa tuhuma nyingi lakini pia akilindwa si jambo jema. Anawakumbusha Takukuru kuyafanyia kazi madai kuwa kuna rushwa imetolewa kwa vile Slaa anaweza kuwa ushahidi na kutibitisha au kukanusha tuhuma hizo.", "\u00a0", "Anaielezea hatua ya kuwatukana maaskofu kama kuporomoka kwa maadili kwani kumeambatana na matusi ,uongo na masingizio kuwa zaidi ya maaskofu 30 kati ya 34 wa Kanisa Katoliki wamehongwa kiasi kikubwa cha fedha.", "\u00a0", "Yapo maelezo mengine kuwa viongozi wa madhehebu mengine wamepewa rushwa na Askofu Josephat Gwajima, anaunganishwa na rushwa jambo ambalo lina lenga kuchafua kanisa na waumini.", "\u00a0", "\u201cHali ya kuporoka maadili ndani ya jamii na heshima kushuka miongoni mwa baadhi ya wanasiasa kunanilazimisha kukumbushana kuwa kuna maisha na urafiki baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi ujao hivyo tunapaswa kuchunga kauli za vinywa vyetu ili kuepusha kuwa na maadui wa kisiasa na hata wa maisha yetu.\u201d", "\u00a0", "Anaeleza kuwa kusema uongo dhidi ya watu fulani kunaweza kujenga uadui na kuhamasisha hasira ndani ya jamii hivyo kuwa chanzo cha vurugu na visasi si baina ya watu lakini hata miongoni mwa wanasiasa.", "Anasisitiza kuwa kila jambo linaloonekana mbegu yake ni \u2018mawazo\u2019 ambayo huwa \u2018maneno\u2019, hivyo kuchunga ulimi ni jambo muhimu kuliko kingene chochote kwa kuwa kauli jambo linatokea.\u00a0"], "byline": ["Na Gaudensia Mngumi\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Wanasiasa kuna maisha zaidi baada ya uchaguzi-Mwamalanga"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84241", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:00.068972"},
{"body": ["Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Alhaj Ally Rufunga, amewataka wadau wa soka wa mkoa huo kuwa kitu kimoja linapiokuja suala la kutafuta mafanikio ya timu zao mbili zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara.", "\u00a0", "Shinyanga inawakilishwa kwenye ligi hiyo ya juu zaidi nchini na timu za Stand United na Mwadui FC na Alhaj Rufunga anaamini kwamba soka la mkoa huo linaweza kuinuka zaidi kama kutakuwa na umoja.", "\u00a0", "Alhaj Rufunga katikati ya wiki wakati wa mechi ya kirafiki kati ya timu ya Olimpique Stars ya Burundi dhidi ya Mwadui FC, ambako sapoti haikuonekana kubwa kwa wenyeji tofauti na Stand United ilipowakabili Warundi hao.", "Rufunga alisema kuwa mashabiki wa soka mkoani Shinyanga wanaweza kufanya soka la mkoa huo kuinuka zaidi na kuwa ajira kubwa kama kutakuwa na umoja.", "\u00a0", "Alisema Stand United inayodhaminiwa na mwekezaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Acacia ya Buzwagi mjini Kahama na Mwadui inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya almasi ya Mwadui Williamson Diamond Ltd zote za mkoani hapa, zinaweza kuwa na mafanikio makubwa zaidi ya kushiriki ligi kuu.", "\u00a0", "Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, wakati umefika sasa kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kutambua kuwa timu zote ni zao na hakuna sababu ya kuwa na ushabiki wa makundi kwa kuiangusha timu nyingine.", "\u00a0", "Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa chama cha soka mkoa wa Shinyanga, Mbasha Matutu, alisema kuwa kuwapo kwa hali ya ushabiki dhidi ya timu fulani ni jambo lisiloepukika katika soka kwani ndilo linalodumisha soka na hiyo ndiyo siri ya mafanikio ya Simba na Yanga.", "\u00a0"], "byline": ["Na Anceth Nyahore\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Stand United, Mwadui zatakiwa umoja."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84250", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:00.533569"},
{"body": ["Kocha wa Ndanda FC, Hamimu Mawazo, ametambia umadhubuti wa safu yake ya ulinzi kuelekea mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mgambo Shooting ya Tanga kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona leo.", "\u00a0", "Mawazo alisema safu imara ya ulinzi inasaidia kutoruhusu idadi kubwa ya magoli na hivyo kuamsha morali ya washambuliaji kutafuta mabao kwa nguvu zaidi.", "\u00a0", "\u201cMwaka huu tuna bahati kwamba maeneo yale yamepata marekebisho mazuri kwenye timu, ninaamini tutakuwa na timu nzuri ambayo itakuwa na uwezo wa kufunga na ninaamini nina mabeki wazuri wenye uwezo mkubwa... maeneo hayo mawili yakifanikiwa tutashinda,\u201d alisema.", "\u00a0", "Alisema, kuhusu changamoto zingine za nje ya uwanja wanazokumbana nazo wachezaji, amekaa nao na kuzungumza nao ambapo wameonyesha kukubali na wote kuwa na lengo moja la ushindi kuelekea katika mchezo huo ambao ni miongoni mwa michezo saba ya ligi kuu inayochezwa leo.", "\u00a0", "Nahodha wa Ndanda, Wilbert Mweta, aliwataka wachezaji wenzake kucheza kwa ushirikiano na kujituma zaidi huku wakifuata maelekezo ya mwalimu wao ili kufanikisha azma yao ya kuondoka na poiti tatu katika mchezo huo.", "\u00a0", "\u201cWachezaji wenyewe tujitume na tushirikiane uwanjani, tufuate maelekezo ya walimu wetu na ninaamini tutayafuata kwasababu tumejiandaa muda mrefu... jambo jingine la msingi ni kwamba mashabiki wetu wajitokeze waje kutusapoti kwasababu tupo katika uwanja wetu wa nyumbani ili tupate hamasa kubwa,\u201d alisema.", "\u00a0"], "byline": ["Na Juma Mohammed\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Kocha Ndanda atambia ulinzi."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84249", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:01.556271"},
{"body": ["Rais Jakaya Kikwete ameshangaza baadhi ya wachunguzi wa habari alipoelekea kutofautiana kwa wazi na waziri wake wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kuhusu kinachoendelea hapa nchini.", "\r\n", "\r\nWalizungumzia mambo mawili tofauti lakini kwa kanuni za hesabu za mwambatano (simultaneous equations) ilikuwa ni kama JK anajibu alichosema Membe, akiwaasa waangalizi wa uchaguzi mkuu kutoka nchi za nje, asasi za kimataifa na za hapa nchini, kuheshimu sheria, taratibu na kanuni.", "\r\n", "\r\nWaziri Membe alizungumza kana kwamba sheria, taratibu na kanuni hizo ndizo zinazowaongoza katika jukumu lao, wakati si hivyo.", "\r\n", "\r\nMembe aliwaambia waangalizi wasifanye mikutano na wanahabari, wasiingilie majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutangaza matokeo na wasifungamane na upande wowote.", "\r\n", "\r\nWaziri Membe anafahamu fika kuwa waangalizi wa uchaguzi mkuu wanaongozwa na itifaki na protokali za kimataifa ambazo Tanzania imezisaini na kuridhia zikaingizwa katika mtiririko wa sheria na hivyo zinaibana kisheria, nje ya zile ambazo imezitunga yenyewe.", "\r\n", "\r\nKwa maana hiyo mtu akikiuka kwa undani kanuni za kimataifa za uchaguzi huru na haki, hawezi kujitetea kwa rejea ya chochote kile kilicho katika sheria za nchi yake badala yake zile za kimataifa zinachukua mkondo wake. ", "\r\n", "\r\nWala hatakuwa na mahali pa kujificha nilazima afikishwe kwenye Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC) ambayo nchi nyingi za Afrika zimekuwa zinaipinga.", "\r\n", "\r\nIwapo taifa litamficha mtuhumiwa wa kukiuka haki za binadamu katika uchaguzi mkuu Marekani italazimisha nchi nyingine kuisusia.", "\r\n", "\r\nKwa njia hiyo matamshi ya Waziri Membe yangeweka mazingira ya kuingiliana na waangalizi wa kura kutoka nje, kama ambavyo mtu wa karibu sana na Membe, katibu mwenezi wa CCM, Nape Nnauye, alivyowahi kusema kuwa CCM itashinda, hata kwa \u2018goli la mkono.\u2019 ", "\r\n", "\r\nEndapo \u2018goli\u2019 kama hilo lingezua mzozo ambako watu 500 au zaidi wanakufa, mazingira ya kuitwa ICC\u00a0 kwenye mahakama kimataifa yangekuwa yameandaliwa na walio madarakani sasa ndiyo wangepata taabu, kujibu mashtaka ya njama za kuharibu uhesabu wa kura, kupotosha matangazo, na kubaka demokrasia. Si rahisi upone kutinga The Hague kwenye korti hiyo.", "\r\n", "\r\nTena kuja matatizo mengine yaliyotangulia ambayo JK anafahamu yanaweza kuibuliwa upya endapo kutakuwa na makosa makubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, yaani kuvurugwa kwa uchaguzi mkuu Zanzibar, kukataza maandamano na kuua watu wanaokisiwa kuwa ni 69, kwa mujibu wa balozi wa Sweden nchini humo wakati huo, Sten Rylander.", "\r\n", "\r\nRais mstaafu Benjamin Mkapa akiwa safarini akasema waliokufa ni\u00a0 17 pekee halafu Tume ya Kisanga ikafikia tamati kuwa waliokufa walikuwa 39.", "\r\n", "\r\nWakati huo ICC haikuwepo na labda, kama anavyosema Ben, labda kama walikuwa 17 tu ICC isingehangaika sana!", "\r\n", "\r\nKwa maana hiyo tamko la JK kuzitaka nchi za Afrika kuacha kuisakama mahakama hiyo ya kimataifa, wakati haijaita hata mwezi alidai kuwa chombo hocho kimesheheni upendeleo dhidi ya Afrika, ni kielelezo kuwa asingetaka kupambana nayo hapo mbeleni.", "\r\n", "\r\nNi kuwaonya wenye hisia kama za Membe na Nape kuwa yeye binafsi anataka afikishe nchi katika tamati salama ya uchaguzi mkuu, astaafu kwa amani bila vikwazo vipya vya safari, au afanye safari ya aibu kwenda The Hague.", "\r\n", "\r\nNa kutokana na yale ya 2001 ambako yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ben ndiye angetajwa kwanza, labda na Amani Karume.", "\r\n", "\r\nKubadilika kwa hisia ya JK kuhusu nafasi ya ICC kama taasisi ya kimataifa, tena baada ya kujiunga na wengine katika Umoja wa Afrika haijapita hata mwezi kuisema taasisi kuwa ina upendeleo uliokithiri dhidi ya nchi za Afrika. ", "\r\n", "\r\nAngebaki hapo kihisia, akarudia kuikandia ICC kama mwanzo, basi angekuwa katika masafwa yale yale na wasaidizi wake hao wawili, Membe na Nape.", "\r\n", "\r\nIla kwa kujitofautisha ametoa ishara ya kudhamiria kufuata sheria, taratibu na kanuni halisi za uchaguzi huru na hai wa kidemokrasia."], "byline": ["Na Miki Tasseni\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["JK aashiria kukwepa mtego wizi wa kura"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84276", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:01.891270"},
{"body": ["Nimefuatilia kwa karibu sana ahadi za wagombea wa kinyang'anyiro cha urais, wagombea wa vyama mbalimbali kwanza nikashangaa na kushindwa kuelewa kama baadhi ya ahadi zao zimefanyiwa uchambuzi au umekuwa ni ushindani wa kutamka ahadi tu.", "\r\n", "\r\nMwamko wa wananchi wa kuwasikiliza wagombea nafasi za uongozi wa juu kwenye kampeni mwaka huu umekuwa mkubwa kuliko chaguzi nyingine zilizopita, katika kila mkutano wa kampeni wa vyama wananchi hujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kusikiliza sera na ilani za vyama husika.", "\r\n", "\r\nKinachojitokeza zaidi katika kampeni hizo ni ahadi zaidi, baadhi ya wagombea wanatoa ahadi ambazo hata ndani ya ilani ya vyama vyao hazimo, na mbaya zaidi ukizisikiliza kwa umakini, utagundua kuwa baadhi hazitekelezeki.", "\r\n", "\r\nAhadi nyingi zimeelekezwa kuwawezesha makundi ya vijana, ambao wameahidiwa kupewa kipaumbele katika kujikwamua na maisha haya ya kukosa ajira pamoja na kujiajiri kwa misingi ya kuwezeshwa, suala ambalo kimsingi kama likitekelezwa kulingana\u00a0 na ahadi hizo, litainufaisha nchi kiuchumi.", "\r\n", "\r\nKimsingi, suala la kutoa mikopo kwa makundi ya vijana wa nchi nzima linaonekana siyo rahisi kutekelezeka, yapo makundi ya vijana lukuki katika kila pembe ya nchi hii, na siyo rahisi kuyabaini kwa uhakika yaliko makundi hayo na kuyafanyia upembuzi kwa ajili ya mikopo iliyokusudiwa.", "\r\n", "\r\nMoja ya ahadi zilizotolewa na mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama cha Tanzania Labour (TLP), Maxmillan Lyimo kwamba akipata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu, atahakikisha makundi yote ya jamii yanapewa mikopo, ambayo alisema itaweza kufuta machungu ya ukosefu wa ajira.", "\r\n", "\r\nAlisisitiza kuwa \"Nataka nimalize kabisa tatizo la ajira ambalo linaitesa nchi yetu kwa miaka 52 sasa, mkinipa ridhaa ya kuunda serikali ya awamu ya tano nitaweka utaratibu wa kuyawezesha makundi yote kupata mikopo kuanzia ngazi ya vijiji...\"", "\r\n", "\r\nWapo pia wagombea wengine ambao ukizingatia uwezo wa kutekeleza ahadi wanazozinadi kwa wananchi unatambua kirahisi kuwa hapa ni sawa na porojo tu, na kwa bahati mbaya ahadi zote zinahitaji uwezo mkubwa wa kifedha, suala ambalo linaibua waswali mkubwa kuwa fedha hizo ziko wapi?", "\r\n", "\r\nNadharia ya madai kuwa nchi hii ni tajiri kutokana na kuwepo kwa rasilimali nyingi, inaweza kuwapotosha wananchi wenye matarajio ya kujinasua na umaskini kutokana na hotuba za ahadi lukuki kutoka kwa wagombea wetu. ", "\r\n", "\r\nUtajiri uliopo si wa kufukua 'mapesa' mahali na kuyagawa kwa wahitaji, ni utajiri wa kimchakato unaohitaji kuainisha vyanzo vyote vya mapato kuanzia madini, gesi, utalii, bahari na maziwa, nk na kuwekeza kitaalamu kwa gharama nyingine kubwa, ndipo upate mapato halisi, na hatua zote hizo zinachukua muda mrefu, si za muda mfupi.", "\r\n", "\r\nWananchi wanahitaji nguvu ya serikali katika miradi inayowanufaisha wote kwa ujumla, wanahitaji elimu bora, huduma za afya, ubora wa miundombinu mbalimbali, viwanda nk. Hayo ni rahisi kuyatekeleza ingawa pia si kwa mara moja.", "\r\n", "\r\nAhadi zinazotolewa kwenye kampeni zilenge matarajio ya maendeleo ya haraka kwa wote, inawezekana hata mikopo ikasaidia lakini kuwepo na viwango pamoja\u00a0 na mipaka yake ili hata udhibiti wa mikopo hiyo uwe rahisi, sidhani kama ni rahisi kuwakopesha wananchi wote nchi nzima!", "\r\n", "\r\nWagombea wakumbuke kuwa ahadi zao zitakuja kugeuka kuwa deni, na wakati mwingine linakuwa ni deni lisilolipika, madhara yake ni kwa wananchi kutokuwa na imani na viongozi hao pamoja na chama husika. ", "\r\n", "\r\nNaelewa kuwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani ni raia halali wa nchi hii, na wanaona na kutambua mambo ya kimaendeleo yaliyofanywa na chama tawala, hata kama hawaridhiki na yaliyofanyika, lakini wao pia ni sehemu ya mafanikio au mapungufu ya malengo ya miradi mbalimbali iliyowekwa na chama tawala, inawalazimisha waitambue.", "\r\n", "\r\nSera na Ilani za vyama hulenga kuboresha huduma bora kwa wananchi wote, vyama vitakavyokosa ridhaa ya wananchi ya kuongoza dola, vinalazimika kutekeleza ilani itakayoanza kutekelezwa na chama kilichoshinda, hii ni Tanzania yetu wote, suala la msingi ni kuwaahidi wananchi maendeleo ya kweli tu.", "\r\n", "\r\n"], "byline": ["Na Owden Kyambile\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Wagombea, ahidini kinachotekelezeka!"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84273", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:01.927837"},
{"body": ["Wakati \u00a0Simba wakipania kuvunja mwiko wa kutopata ushindi kwenye uwanja wa Mkwakwani kwa misimu mitatu mfululizo watakapokabiliana na African Sports leo, nyota wa kimataifa wa Yanga wakiwamo, Donald Ngoma, Amisi Tambwe na Thaban Kamusoko kesho watashuka kwenye Uwanja wa Taifa wakati timu yao ikiumana na Coastal Union ya Tanga baada ya mabingwa hao kukamilisha taratibu zote za usajili wa nyota hao.", "\u00a0", "Awali, kulikuwa na hofu kukosa vibali kwa nyota hao wa Yanga baada ya klabu hiyo ya Jangwani kutishia kugomea kuwalipia ada ya dola 2,000 kwa kila nyota wa kigeni kama kanuni mpya za ligi zinavyoagiza.", "\u00a0", "Hata hivyo, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Jonas Tiboroha, ameiambia Nipashe kuwa wamekamilisha taratibu zote na wachezaji hao wapo tayari kwa mchezo wa kesho.", "\u00a0", "Tiboroha aliwataka mashabiki wa klabu hiyo kuondoa hofu ya kuwakosa wachezaji hao na kusema wamemalizana na TFF juu ya malipo ya nyota hao.", "\u00a0", "\"Wachezaji hawa wataichezea Yanga kuanzia Jumapili, tumekamilisha kila kitu hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi juu yao,\" alisema Tiboroha.", "\u00a0", "Hata hivyo, Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, alisema kuwa hakuwa na taarifa za kukamilika kwa taratibu zote za wachezaji Yanga na kusema kuwa kama imefanyika hivyo watakuwa wapo huru kuichezea timu yao.", "\"Kama Yanga wamefanya hivyo wachezaji wake watakuwa huru kuichezea, kwa sasa nipo nje ya ofisi sina taarifa kamili,\" alisema Kizuguto.", "\u00a0", "Uwapo wa wachezaji hao utachangia kwa kiasi kikubwa Yanga kuingia uwanjani huku ikiwa na matumaini ya ushindi kama kocha wake, Hans van der Pluijm alivyoiambia Nipashe.", "\u00a0", "\"Nahitaji kuwa na wachezaji wangu wote.., hii itananipa wigo mpana wa kupanga timu yangu katika mchezo wa Jumapili,\" alisema Pluijm.", "\u00a0", "Yanga itaingia uwanjani kesho, ikiwa na kumbukumbu ya kuisambaratisha Coastal kwa magoli 8-0 katika mechi yao iliyopita kwenye uwanja huo, huku Tambwe akitupia mabao manne.", "\u00a0", "Simba itajaribu kuvunja mwiko wa kutopata ushindi kwa misimu mitatu mfululizo kwenye uwanja wa Mkwakwani itakapoumana na African Sports leo.", "\u00a0", "Tangu 2011 ilipofungiwa bao la mwisho ya Patrick Mafisango, Simba haijapata goli hata moja kwenye Uwanja wa Mkwakwani tangu wakati huo ambako imekuwa ikiambulia sare au vipigo.", "\u00a0", "Kocha wa Simba, Dylan Kerr, amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha timu yake inaanza kwa ushindi katika mchezo huo wa leo.", "\u00a0", "Simba inaumana na African Sports wakitokea visiwani Zanzibar ambako kwa kipindi cha wiki mbili walikuwa wameweka kambi kujiandaa na ligi kuu."], "byline": ["Na Faustine Feliciane\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Simba kama mbwai mbwai."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84247", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:02.050673"},
{"body": ["Kocha wa timu ya Simba, Dylan Kerr, amesema tatizo linalokwamisha maendeleo ya soka la Tanzania ni kukosekana kwa wafungaji.", "\u00a0", "Muingereza huyo amesema kama timu mojawapo ya Tanzania ingekuwa na wamaliziaji wazuri, wangekuwa wanaona ligi nyepesi sana.", "\u00a0", "Akizungumza baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga juzi, Kerr alisema: \u201cTatizo la Tanzania ni wafungaji. Kama ukiwa na wafungaji wazuri ligi ingekuwa nyepesi sana.\u201d \u00a0 \u00a0", "\u00a0", "Simba ilipata ushindi wa kwanza na goli la kwanza Mkwakwani tangu Agosti 24, 2011 kupitia Mganda Hamis Kiiza na Kerr amesema wachezaji wake walicheza kwa kiwango cha juu licha ya tatizo katika umaliziaji. Mchezaji wa mwisho kuifungia Simba Mkwakwani alikuwa Patrick Mafisango katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union 2011.\u00a0", "\u00a0", "\u201cNina furaha sana kwa ushindi huu ambao umevunja rekodi ya Simba kutoshinda kwa miaka minne kwenye uwanja huu, nimefurahishwa na kila wachezaji kwa kufanya kazi yake vizuri, Kiiza pia kwa kufunga bao pekee na Majabvi kucheza vizuri nafasi ya ulinzi leo (juzi),\u201d alisema Kerr.", "\u00a0", "Kocha huyo aliongeza ataendelea kuwaboresha washambuliaji wake ili waweze kufunga zaidi katika mechi zinazofuata.", "\u00a0", "\u201cSiijui Mgambo, ila katika maandalizi tuliyofanya ilikuwa ni kuimarisha timu kwa lengo la kupambana na yeyote atakayekuja, \u00a0naamini tutakuwa tofauti zaidi ya leo kwa sababu kila mchezo una mkakati wake,\u201d Kerr alisema.", "\u00a0", "Aliongeza kwamba anaahidi kasi ya timu yake itaongezeka na mechi ya keshokutwa Jumatano pia itakuwa na ushindani.", "\u00a0"], "byline": ["Na Somoe Ng`itu\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Kerr: Tatizo Tanzania hamna wafungaji."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84310", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:02.084432"},
{"body": ["Tanzania imeendelea kufanya vibaya kwenye michezo ya Afrika (All Africa Games) inayoendelea nchini Kongo Brazaville baada ya bondia, Hamadi Furahisha, kutupwa nje kwenye michezo hiyo.\u00a0", "\u00a0", "Bondia huyo alipokea kipigo kutoka kwa bondia wa Angola na hivyo kutupwa nje ya michezo hiyo.", "\u00a0", "Furahisha ambaye alipata bahati ya kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo kwa ushindi wa chee kutokana na mpinzani wake kushindwa kutokea wakati wa kupima uzito na kuchelewa kupanda ulingoni katika mchezo wa kwanza, alijikuta akipoteza pambano baada ya kupigwa kwa pointi dhidi ya bondia huyo raia wa Angola.", "\u00a0", "Matokeo hayo yanamaanisha kuwa mabondia wote watatu wa Tanzania wameaga michezo hiyo.", "Bondia wa kwanza kuaga michuano hiyo ni Ismail Geriatano, ambaye alipigwa na bondia kutoka Algeria, akifuatiwa na Said Hofu aliyetolewa kwa KO na bondia kutoka nchini Ghana.", "\u00a0", "Mbali na mabondia wanamichezo wengine wa Tanzania ambao wametolewa katika michuano hiyo ni wa mchezo wa kuogelea pamoja na timu ya soka ya wanawake ya 'Twiga Stars' iliyofungwa \u00a0mechi mbili za kwanza.", "\u00a0", "Katika michezo hiyo, Tanzania imebakiwa na wanamichezo katika michezo ya riadha, judo na Paralimpiki, ambayo wachezaji wake wanatarajia kuanza kutupa karata zao kesho."], "byline": ["Na Renatha Msungu\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Tanzania yazidi 'kuchemsha' Afrika."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84248", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:02.314400"},
{"body": ["Simba jana ilivunja mwiko wa kutopata ushindi kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Sports, shukrani kwa mshambuliaji Hamis Kiiza aliyefunga bao pekee kwenye mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu na kupeleka pointi zote tatu Msimbazi.", "\r\n", "\r\nSimba haijawahi kupata ushindi kwenye Uwanja wa Mkwakwani kwa miaka mitatu mfululizo na ushindi wa jana ni kama alama ya mafanikio.", "\r\n", "\r\nKiiza alitikisa kamba za Sports kwa kichwa katika dakika ya 56, akimaliza krosi kutoka kwa nahodha wa Wekundu hao wa Msimbazi, Mussa Hassan \u2018Mgosi\u2019. ", "\r\n", "\r\nKatika mchezo huo, ilionekana kama vile Sports wanataka kuendelea kuibana Simba ili ishindwe kutibu \u2018majeraha\u2019 ya kutopata ushindi kwenye uwanja huo baada ya kufanya shambulizi kubwa dakika mbili tangu kuanza mchezo.", "\r\n", "\r\nMshambuliaji Pera Maveo angeweza kufanya matokeo kuwa 1-0 kama siyo shuti lake kali kupaa juu ya lango la Simba, akiwa ndani ya eneo la hatari kufuatia pasi ya kiungo Novat\u00a0 Lufungo.", "\r\n", "\r\nSimba walijibu shambulizi hilo dakika mbili baadaye kupitia kwa Mzimbabwe, Justive Majabvi ambaye mpira wake wa kichwa kufuatia krosi ya Awadhi Juma kuchezwa vizuri na mlinda mlango wa African Sports, Yusuph Yusuph.", "\r\n", "\r\nKiiza alikaribia kuifungia Simba goli la kwanza, lakini shuti lake lilidakwa na kipa Yusuph kuelekea robo ya dakika 45 za kwanza.", "\r\nKipa wa Simba, Manyika Peter alifanya kazi ya ziada kuicheza vizuri mikwaju miwili ya kushtukiza kutoka kwa Hussein Amri na Hassan Matemena.", "\r\n", "\r\nDakika ya 38, Matemana alikaribia kuleta balaa Msimbazi kama siyo shuti lake kushindwa kulenga shabaha lango la Simba akiwa yeye na kipa na kufanya dakika 45 kumalizika bila nyavu kutikisika.", "\r\n", "\r\nSimba walianza kipindi cha pili kwa kupoteza nafasi ya wazi kufunga kupitia Mgosi aliyepiga shuti \u2018cha mtoto\u2019 lililoshindwa kumpa tabu kipa Yusuph.", "\r\n", "\r\nDakika ya 89 African Sport walipata nafasi ya kusawazisha goli hilo, kama siyo papara za kutaka kufunga bila umakini kwa mshambuliaji Hussein Ali.", "\r\n", "\r\nKatika viwanja vingine, Azam FC ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo kwenye Uwanja wa Azam Complex, kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Mtibwa waliibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Stand United, wakati kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara Ndanda FC walilazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Mgambo JKT.", "\r\n", "\r\nKwenye Uwanja wa Sokoine, wenyeji Mbeya City walishangazwa na Kagera Sugar baada ya kukubali kipigo cha goli 1-0.", "\r\n", "\r\nToto African walitumia vizuri uwanja wa nyumbani, CCM Kirumba kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwandui ya Shinyanga, huku Nizar Khalfani akikosa penati kwa upande wa Mwadui katika dakika ya 60.", " Manyika Peter, Mohamed Hussein \u2018Tshabalala\u2019, Hassan Kessy, Juuko Mursheed, Justive Majabvi, Awadh Juma, Said Ndemla,\u00a0 Mwinyi Kazimoto, Mussa Hassan \u2018Mgosi\u2019, Hamis Kiiza/Boniface Maganga (75), Peter Mwalyanzi.", "\r\n", "\r\n", " Yusuph Yusuph, Ayoub Masoud, Mwaite Gereza, Juma Shemvuni, Rahim Abdallah, Novat Lufungo, James Mendi/Ally Ramadhan (83), Hussein Amir, Hassan Matemema, Omari Issa,\u00a0 Pera Maveo.", "\r\nImeandikwa na Somoe Ng\u2019itu (Tanga), Daniel Mkate (Mwanza), Devotha Kiwhelu (Dar), Marko Maduhu (Shinyanga)"], "byline": ["Na Waandishi wetu \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Simba yavunja mwiko wa ushindi Mkwakwani"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84277", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:02.732931"},
{"body": ["Mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samata amefunga mabao matatu katika ushindi wa TP Mazembe Englebert wa 5-0 dhidi ya timu ya Moghreb Tetouan ya Morocco na kuwapeleka miamba hao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye nusu-fainali ya Ligi ya mabingwa wa Afrika.", "\u00a0", "Timu hizo zilienda katika mechi hiyo ya mwisho ya Kundi A juzi zikiwa na pointi sawa, lakini mabao ya straika huyo kipenzi cha Watanzania yaliwasambaratisha kabisa Wamoroco hao.", "\u00a0", "Mazembe wamejumuika katika nusu-fainali pamoja na klabu ya Al Hilal baada ya Nasreldin Al Shigail kufunga goli katika dakika ya 75 na kuwapa Wasudan hao sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Smouha ya Misri.", "\u00a0", "Al Hilal walimaliza wa pili katika Kundi A na kuungana na Wasudan wenzao, Al Merreikh, ambao walimaliza wa pili katika Kundi B, kutinga nusu-fainali.", "\u00a0", "Kina Samata TP Mazembe watawakabili Al Merreikh wakati Al Hilal watawavaa vinara wa Kundi B, USM Alger ya Algeria katika nusu-fainali.", "\u00a0", "Vinara wa makundi wanaanzia ugenini Okt. 3-4, wiki moja baada ya mechi za kwanza kuchezwa.\u00a0"], "byline": ["Na Waandishi wetu \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Samata atupia 'hat-trick' Afrika."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84309", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:03.062172"},
{"body": ["Kwa upande wake, Masaburi alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, simu yake haikuwa hewani na alipotumiwa ujumbe wa maandishi haukujibiwa.\u00a0", "Umoja wa wafanyabiashara Soko la Machinga Complex, jijini Dar es Salaam, umeeleza kusikitishwa na tetesi za kuuzwa kwa jengo hilo kwa mwekezaji kutoka China hivyo kumwomba Rais Kikwete, kuingilia kati kabla hajaondoka madarakani.", "\u00a0", "Tetesi hizo zilibainishwa jana na Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Gerald Mpangama, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya soko hilo na kupinga taarifa aliyodai kutolewa na Meya wa jiji hilo, Dk. Didas Masaburi, kwamba hatambui upangaji wa shule ya Lamoon kwenye jengo hilo.", "\u00a0", "Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, suala la uuzwaji wa jengo hilo lililojengwa kwa mkopo na Shirika la Hifadhi la Jamii (NSSF), kwa Sh.bilioni 12, lilijadiliwa katika kikao chake cha bodi hivi karibuni.", "\u00a0", "Alisema wafanyabiashara hawako tayari kuona jengo hilo, ambalo lilijengwa na serikali kwa ajili ya kupunguza changamoto ya maeneo ya kufanyia biashara kwa wafanyabiashara ndogondogo \u2018machinga\u2019, likiuzwa.", "\u00a0", "\u201cSisi wafanyabiashara wa Machinga Complex, tunasema msimamo wetu utakuwa palepale kwamba jengo hili lilijengwa na serikali kwa ajili ya kutatua au kupunguza suala zima la maeneo ya kufanyia biashara kwa wafanyabiashara wadogowadogo nchini,\u201d alisema na kuongeza:", "\u00a0", "\u201cTunaomba serikali kupitia Rais wetu, ambaye kwa nia na dhamira yake nzuri kwetu sisi na wafanyabiashara wadogo wa Machinga Complex, tunamuomba alizungumzie suala hili la uuzwaji wa jengo letu la Machinga Complex na kulitolea ufafanuzi katika moja ya hotuba zake za mwezi kabla hajaondoka kwenye kiti chake cha urais.\u201d", "\u00a0", "Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, hawajashirikishwa wala hawajui mauzo yake yataanza lini japokuwa tayari wameshabaini mwekezaji kutoka China akija \u00a0kupiga picha jengo hilo kwa madai ya mauzo ya takribani Sh. bilioni 38.", "\u00a0", "Kuhusu kupangishwa kwa shule hiyo katika jengo hilo, Mpangama alisema anayehusika kutia sahihi ya mkataba huo ni halmashauri ya jiji, ambao ndio wenye jengo na wala hakuna mahali popote katika nyaraka zake panapomruhusu meya wa jiji kuweka sahihi.\u00a0", "\u00a0", "Akijibu malalamiko hayo, Mkurugenzi wa jiji hilo, Wilson Kabwe, alisema hana taarifa yoyote ya kuuzwa kwa jengo hilo, lakini wapo katika mazungumzo na NSSF kuhusu urejeshwaji wa deni hilo ambalo kwa sasa limefikia Sh. bilioni \u00a034 kutoka Sh. bilioni 12.", "\u00a0"], "byline": ["Na Isaya Kisimbilu\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Wamachinga wamlilia JK kuuzwa Machinga Complex."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=80907", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:03.608763"},
{"body": ["Alisema hivi sasa benki hiyo ina matawi 163 na mashine za ATM 500 nchi nzima zinazowezesha wateja wake kupata huduma kwa urahisi.\u00a0", "Benki ya NMB imetenga Sh. bilioni 52 kama gawio la hisa kwa wanahisa wake mwaka huu ikiwa ni sawa na gawio la Sh. 104 kwa kila hisa moja.", "\u00a0", "Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, alisema benki hiyo imeendelea kufanya vizuri mwaka uliopita kwa kupata faida ya Sh. bilioni 155.6 baada ya kodi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16 ikilinganishwa na faida Sh. bilioni 134 mwaka juzi.", "\u00a0", "Alisema kutokana na mafanikio hayo, NMB inakusudia kuingia kwenye mfumo wa mastercard ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma za kifedha ndani na nje ya nchi kwenye benki yoyote.", "\u00a0", "Naye Mkurugenzi wa Fedha, Waziri Barnabas, NMB imerejesha huduma za mikopo kwa wateja wake wakiwamo watu binafsi, vikundi na kampuni.", "\u00a0", "\u201cTunaendelea kupanua huduma zetu na sasa tunakusudia kuanzisha NMB wakala ili wateja wetu waweze kupata huduma kwenye maeneo ambayo bado hatujafika,\u201d alisema.", "\u00a0"], "byline": ["Na Restuta James\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["NMB yatenga gawio la hisa bilioni 51/-"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=81038", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:03.615663"},
{"body": ["Leo nitajadili kuhusu udhibiti wa mali (stock control). Yafaa kukumbuka kuwa, ukinunua \u00a0mali kwa ajili ya biashara yako unahitaji kuidhibiti ili iweze kutoa matokeo mazuri ya kibiashara.", "\u00a0", "Udhibiti wa mali (stock control) maana yake ni utaratibu katika biashara unaohusisha upokeaji mali, uwekaji kumbukumbu wa mali, uhifadhi wa mali, upangaji wa mali, uhakiki wa mali na uagizaji wa mali.", "\u00a0", "Makala iliyopita \u00a0ilizungumzia moja ya tatizo kubwa linalowakabili \u00a0ni kuhusu kutokutunza kumbukumbu za biashara, walikumbushwa kuwa mali bila daftari hupotea bila habari, huwezi kukumbuka kil akitu juu ya shughuli zako za kila mara.", "\u00a0", "Udhibiti wa mali ni muhimu katika biashara, kwani husaidia kufahamu ni wakati gani, vipi na kwa nini unahakikisha huishiwi mali ili usiwakere wateja wako. Pia itakusaidia kupunguza hasara inayoweza kusababishwa na wizi, uharibifu au uchakavu.", "\u00a0", "Udhibiti wa mali, husaidia biashara kuainisha aina za bidhaa na vitu ambavyo wateja wanahitaji. Kwa kuangalia mwenendo wa mtiririko wa mali, unaweza kutofautisha kati ya bidhaa zinazotoka haraka na zile zinazotoka taratibu.", "\u00a0", "Mali katika biashara inadhibitiwa kwa kuweka kumbukumbu sahihi. Kwa mfano kuweka kadi za mali, orodha ya mali, ankara na kumbukumbu za mauzo taslimu za kila siku katika biashara yako.Usifanye biashara kwa mazoea kwa kujaza tu duka lako.\u00a0", "\u00a0", "Ili kuwa na udhibiti wa mali wenye kujenga ufanisi, kuna njia mbalimbali wajasiriamali wanakumbushwa kuzizingatia ili kujenga ufanisi katika biashara zao. Njia hizi ambazo hutoa mwongozo wa kudhibiti mali zipo tano, nazo ni kama zifuatavyo:", "\u00a0", "Weka kiasi sahihi cha mali", "Kumbuka kuweka kiasi sahihi cha mali. Mjasiriamali unakumbushwa kuweka kiasi sahihi cha mali, usiweke mali nyingi mno au mali chache. Mali nyingi zinazuia fedha zako zisizunguuke na mali chache zinaweza kwisha na ukasimama katika mauzo.", "\u00a0", "Tunaposema usiweke mali nyingi au chache maana yake, mjasiriamali anapaswa kuzingatia mahitaji ya wateja wake.Mara zote yapasa kufahamu mwenendo wa hitaji la soko lako.Pia mjasiriamali anapaswa kuwa makini katika uagizaji mali.", "\u00a0", "Bidhaa ipi inatoka haraka", "Jiulize bidhaa zipi zina mzunguko mzuri? Mjasiriamali unashauriwa kuelewa utokaji wa bidhaa katika biashara yako.Wajasiriamali wanakumbushwa kuweka bidhaa zinazotoka haraka na hii itafanya mauzo kuwa mazuri, hivyo kuingiza fedha nyingi katika biashara.", "\u00a0", "Kwa kuwa kuna mali zinazotoka taratibu lakini zikiwa zinatoa faida nzuri, yafaa kuweka kiasi kidogo cha mali zinazotoka taratibu ili kukwepa kukwamisha fedha zako katika mali. Vile vile kumbuka kutoa bei zenye punguzo ili kuvutia wateja na kumaliza haraka.\u00a0", "\u00a0", "Unapanga vipi bidhaa zako?", "Jiulize namna \u00a0unavyopanga bidhaa zako au unapanga tu? Kumbuka upangaji mzuri wa bidhaa zako ni namna nzuri ya kuwavutia wateja. Mjasiriamali kupanga bidhaa \u00a0katika hali ya unadhifu itasaidia wateja kuona kwa urahisi pia kurahisisha kuhesabu na kuhakiki.", "\u00a0", "\u00a0", "Tunapozungumzia upangaji wa bidhaa kama njia ya kudhibiti mali, yafaa ieleweke kwamba, kwa bidhaa au vitu vinavyofanana yafaa vionyeshwe au kuwekwa kwa ukaribu, na inapasa kuepuka kuweka mali hasa vitu vinavyoharibika kwa muda mrefu.", "\u00a0", "Fanya ukaguzi wa mali.", "Jijengee utaratibu wa kukagua mali katika biashara yako. Ni muhimu kukagua mali mara kwa mara ili kufahamu kama biashara yako ina bidhaa zinazohitajika na hakuna mali inayokosekana, pia itakusaidia kugundua kama kuna tatizo lolote katika bidhaa.", "\u00a0", "Weka kumbukumbu za mali", "Kumbuka kuweka kumbukumbu za mali. Mjasiriamali yakupasa kuacha kufanya biashara kwa mazoea, jitahidi kuweka kumbukumbu za mali. Hii ni changamoto kubwa inayowakuta wajasiriamali wengi katika biashara, yafaa kuiangalia kwa kirefu zaidi.", "\u00a0", "Kumbukumbu za mali ni maandishi yanayoeleza kilichotokea kwa mali katika biashara. Inamaanisha \u00a0kumbukumbu ya mali inayoingia na inayotoka katika biashara. Kama unahitaji kufanikiwa ni vizuri kujua mwenendo mzima wa mali katika biashara.", "\u00a0", "Yafaa ieleweke kuwa, wajasiriamali wanaweza kuweka kumbukumbu za mali katika nyaraka na namna mbalimbali. Kwa ajili ya kuwakumbusha wajasiriamali, leo tutaangali namna mbili ambazo zimekuwa zikitumika \u00a0kuweka kumbukumbu za mali. Njia hizo ni kadi ya mali na orodha ya kuhesabu mali.", "\u00a0", "Kadi ya mali hutumika kuweka taarifa juu mali. Inahusisha mambo mengi kama vile, jina la mali, bei kununulia, bei ya kuuzia, kiasi kipya cha kuagiza, tarehe ya mauzo, mali iliyotoka na salio."], "byline": ["Na Waandishi wetu \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Udhibiti katika biashara unavyochangia mafanikio."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=83083", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:04.631126"},
{"body": ["Kampuni zinazomilikiwa na mfanyabiashara Yusuph Manji, ni miongoni mwa kampuni kubwa zilizotajwa bungeni kwamba zinakaidi kulipa deni la zaidi ya Sh. bilioni 9 kati ya Sh. bilioni 233 zilizokopwa katika Mfuko wa Uwekezaji Uagizaji Bidhaa Kutoka nje ya nchi (CIS).", "\u00a0", "Kampuni hizo zilitajwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara wakati ikiwasilisha hotuba yake bungeni jana kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016.", "\u00a0", "Mwenyekiti wa kamati hiyo, Luhaga Mpina, alisema kampuni hizo ambazo zipo zaidi ya 980, zimekaidi kulipa deni hilo ambalo sasa limefikia zaidi ya Sh. bilioni 233, zikiwamo kampuni za Manji.", "\u00a0", "Mpina alisema pamoja na kamati kuiagiza Wizara ya Fedha kutayarisha orodha ya madeni inayozingatia malimbikizo ya riba, lakini wizara hiyo ilikaidi na hivyo kipengele cha \u2018compound interest\u2019 kimekokotolewa na watalaamu wa kamati na kuonyesha hali halisi ya deni kuwa ni Sh. trilioni 1.4.", "\u00a0", "\u201cKampuni za Farm Equip (T) Limited na Quality Group Garage zimekuwa zikiendelea kukaidi kulipa deni lake lililofikia Sh.bilioni 9.06, ambazo ni pamoja na malimbikizo ya riba (compounding interest),\u201dalisema.", "\u00a0", "Mpina alizitaja baadhi ya kampuni zenye uwezo wa kulipa madeni hayo lakini zimekuwa zikilipa kwa kusuasua kuwa ni Quality Group Garage ambayo inadaiwa Sh. bilioni 6.81 pamoja na malimbikizo ya riba, Dun Motors Hill Sh. bilioni 9.11,SASA Stell Rolling Sh. bilioni 7.86, na ALAF Sh. bilioni 13.37.", "\u00a0", "Kampuni nyingine ni Universal Electronic and Hardware Sh. bilioni 9.32, African Trade Development Sh.bilioni 5.22 na Sabira Investment Sh.bilioni 6.52.", "\u00a0", "Nyingine ni Dar es Salaam Cottage Industries Sh.3.22, Farm Equip (T) LTD inayodaiwa Sh. bilioni 2.25 na kampuni ya Appolo Freight Carriers ambayo inadaiwa Sh.bilioni 2.24.", "\u00a0", "\u201cKamati inashangazwa na kusikitishwa na jitihada dhaifu za ukusanyaji wa madeni hayo huku serikali ikiendelea kutoza kodi wananchi maskini na kuachia zaidi ya Sh. trioni 1.4, ikiwa ni fedha za umma kumilikiwa na watu wachache kinyemela,\u201dalisema.", "Alisema ukusanyaji wa madeni hayo umesimama tangu Desemba 2012 kutokana na mkataba wa Msolopa Investment Co.Ltd kufika mwisho na hivyo tangu kipindi hicho, hakuna jitihada zozote za ukusanyaji wa madeni hayo.", "\u00a0", "Aliongeza kuwa ukusanyaji dhaifu wa madeni umesababisha wadaiwa kulipa kwa kusuasua na wengine kukaidi kulipa licha ya kuwa wana uwezo na wana dhamana ambazo zinaweza kufilisiwa kulipia madeni hayo.", "\u00a0", "Mpina alisema kamati yake imebaini kuwa baadhi ya kampuni zilipewa mikopo mikubwa zaidi ya kiwango kilichoruhusiwa na baadhi ya kampuni binafsi, viwanda na wafanyabiashara wameripotiwa kuwa hawapatikani wakati wapo nchini na wanaendelea na biashara.", "\u00a0", "JINSI FEDHA HIZO ZILIVYOPATIKANA", "Katika kipindi cha mwaka 1980 hadi 1992/1993, serikali ilikumbwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni kutokana na matatizo ya kiuchumi.", "\u00a0", "Kutokana na hali hiyo, washiriki wa maendeleo walitoa fedha za kigeni kwa mpango maalum uliofahamika kama \u2018Commodity Import Suport\u2019 (CIS), ukilenga kuipatia serikali uwezo wa kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuzipatia taasisi za serikali, kampuni binafsi, viwanda na wafanyabiashara mbalimbali uwezo wa kuagiza bidhaa na malighafi kutoka nje ya nchi.", "\u00a0", "Fedha za CIS zilitolewa kama mkopo na wakopaji walitakiwa kulipa deni hilo bila kutozwa riba ndani ya kipindi cha miezi 18 na baada ya hapo kulipa riba ya asilimia 12.", "\u00a0"], "byline": ["Na Thobias Mwanakatwe\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Wabunge wamkalia kooni Manji kwa kukalia mabilioni ya serikali."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=81040", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:05.015904"},
{"body": ["Serikali imesema mfumo wa soko la bidhaa unaotarajiwa kuanza hapa nchini hivi karibuni, utasaidia kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto za masoko kwa wakulima.", "\u00a0", "Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa mfumo huo unaotarajiwa kuanza mwaka huu, utasaidia wakulima kuwa na soko la uhakika, bei nzuri na inayostahili.", "\u00a0", "Alisema hayo baada ya kufungua warsha iliyolenga kuzungumzia mfumo wa soko la bidhaa, faida na changamoto zake.", "\u00a0", "\u201cNi kwa kufanya hivi ndipo wakulima wataanza kuona kilimo kama biashara nyingine na kufanya maamuzi sahihi ya kuwekeza na hivyo kuimarisha sekta hiyo na kupambana na umaskini,\u201d alisema Balozi Sefue. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi, tayari serikali imeshawekeza fedha nyingi kuhakikisha mfumo huo unaanza nchini ambapo tayari kampuni ya Tanzania Mercantile Exchange Public Limited Company, imeshasajiliwa \u00a0kusimamia mfumo huo.", "\u00a0", "Katika kampuni hiyo, serikali ina asilimia 49 wakati wadau toka sekta binafsi nchini kama ushirika na vyama vya wakulima wana asilimia 51 ya hisa.", "\u00a0", "\u201cSerikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha mfumo huo muhimu unaanza haraka,\u201d alisema. Mfumo huo unawezesha wauzaji na wanunuaji kukutana na kufanya biashara kwa uwazi na kwa kufuata taratibu maalum zilizowekwa.", "\u00a0", "Nchi kama Ethiopia zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza sekta yake ya kilimo na kufaidisha wakulima wake.", "\u00a0", "Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Soko la Mitaji (CMSA), Nasama Massinda, alisema mfumo wa soko la mitaji ni muhimu katika kufanikisha sera ya taifa ya Kilimo Kwanza.", "Alisema kampuni hiyo itaanza na bidhaa zilizo chini ya mfumo wa stakabadhi ghalani kama korosho, alizeti na mpunga.", "\u00a0", "Alisema mfumo huo utasaidia kuleta uwazi, bei nzuri, kupunguza mianya ya rushwa na kuongeza kuaminiana miongoni mwa wadau kwa ujumla.", "\u00a0", "Mshiriki mmoja wapo wa warsha hiyo, James Shimbe, alisema mfumo huo utasaidia kuimarisha vipato vya wakulima.", "\u00a0", "Washiriki wa warsha hiyo walikuwa ni pamoja na maofisa waandamizi wa serikali, sekta binafsi, \u00a0Muungano wa Vyama vya Ushirika, Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) miongoni mwa wengine."], "byline": ["Na Waandishi wetu \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Balozi Sefue-Mfumo wa soko la bidhaa utainua sekta ya kilimo."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=82859", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:05.175408"},
{"body": ["Msimu wa 52 wa Ligi Kuu Tanzania Bara utaanza rasmi Jumamosi, safari hii ukishirikisha timu 16, mbili zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita.", "\u00a0", "Tayari wadhamini wakuu wa ligi hiyo, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wameshakabidhi vifaa kwa timu zote huku wakiongeza mkataba wa miaka mitatu kuendelea udhamini wao huo wenye thamani ya Sh. bilioni 6.7.", "\u00a0", "Tukiwa wadau namba moja wa michezo nchini, Nipashe tunawapongeza Vodacom Tanzania kwa kuendelea kuipa nguvu ligi hiyo kubwa zaidi nchini.", "\u00a0", "Tunaamini timu zote shiriki zimejipanga kufanya vyema msimu huu. Tunatoa rai kwa marefa kuchezesha kwa haki na kwa kuzingatia matakwa ya Sheria 17 za Soka ili washindi wapatikane ndani ya uwanja na si kwenye mazingira ya nje ya dimba.", "\u00a0", "Tunawakumbusha watendaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kujikita katika misingi ya kiuweledi kuhakikisha si tu kwamba haki inatendeka, bali ionekane inatendeka kwa timu zote shiriki ili kulinda udhamini uliopo na kuvutia wadhamini wengine.", "\u00a0", "Nipashe tunatambua kwamba katika misimu iliyopita ligi hiyo ilikumbwa na changamoto ya rushwa na upangaji matokeo. Miezi miwili tulitoa ripoti iliyofichua namna baadhi ya waamuzi, viongozi wa klabu na watendaji wa TFF wanavyoshiriki kwenye kadhia ya rushwa na upangaji matokeo.", "\u00a0", "Tunafahamu pia kuwa shirikisho limeboresha kanuni zake kwa kuongeza adhabu kwa watoa rushwa na wapangaji matokeo ya mechi za soka nchini, lakini bila weledi na usimamizi thabiti, ni wazi kanuni hizo hazitakuwa na umuhimu wowote kwa soka la Tanzania linalozidi kuporomoka.", "\u00a0", "Ratiba ya ligi hiyo imezingatia mechi za kimataifa za timu za taifa, michuano ya Afrika na Kombe la Mapinduzi, hatutarajii kuona ratiba hiyo inapanguliwa mara kwa mara kama ilivyokuwa msimu uliopita kwani utaratibu huo ni miongoni mwa mbinu za kupanga matokeo tulizozifichua.", "\u00a0", "Tunatarajia kuona ligi inapotakiwa kusimama kupisha michuano ya kimataifa, isimame kwa timu zote 16. Pasiwapo na timu inayokuwa na mechi nyingi za viporo kuzidi timu nyingine.", "\u00a0", "Nipashe tungependa kutoona upendeleo wa baadhi ya timu katika utoaji wa adhabu zitokanazo na makosa ya kinidhamu kama ilivyokuwa msimu uliopita ambao nyota wa baadhi ya klabu hawakuchukuliwa hatua kutokana na baadhi ya watendaji wa shirikisho kuwa na maslahi binafsi na klabu husika.", "\u00a0", "Tunasikitika kuona kuwa tunaingia katika msimu mpya ilhali TFF inasita kuwaadhibu baadhi ya nyota wa klabu zinazotajwa kuwa kubwa, licha ya kufunguliwa mashtaka kwenye Kamati ya Nidhamu ya shirikisho.", "\u00a0", "Nipashe tunaamini upendeleo wa aina hii ni hatari kwa soka la Tanzania kwani mbali ya kuwa miongoni mwa mbinu chafu zinazotumika kupanga matokeo, pia unashusha hadhi ya mamlaka husika (TFF) na kuzuia ufadhili na udhamini wa soka nchini. Hakuna kampuni makini duniani \u00a0inayoweza kufadhili au kudhamini taasisi inayolea ubabaishaji katika utendaji.", "\u00a0", "Tunawashauri watendaji wa TFF kuweka kando mapenzi yao kwa baadhi ya klabu ili wasimamie bila upendeleo Kanuni za Ligi za shirikisho kwa kuwa tunaamini pasi na kufanya hivyo, haki haitatendeka kwa timu zote msimu huu maana 'damu nzito kuliko maji'.", "\u00a0", "Tunazitakia kila la kheri timu zote 16 zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu!\u00a0"], "byline": ["Na Editor \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Haki itendeke timu zote 16 Ligi Kuu Bara."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84065", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:05.652498"},
{"body": ["Huku kampeni za kuwania urais, ubunge na udiwani zikiwa zimepamba moto kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu, kumejitokeza viashiria vya baadhi ya wanasiasa kuanza kutoka nje ya mstari na kwa kufanya \u00a0kampeni kwa misingi ya udini, ukabila na ukanda.", "\u00a0", "Hali hii inatishia amani na utulivu ambavyo vimekuwa tunu adhimu ya taifa hili tangu Tanzania Bara ilipopata uhuru wake mwaka 1961 na baada ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.", "\u00a0", "Mambo yanayojitokeza sasa yanatishia kuweka nyufa katika taifa letu ambalo kwa miaka mingi limejizolea sifa ya kuwa na amani ya utulivu. Tunakemea vikali kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wagombea, wanasiasa na wapiga debe kutaka wapigakura kuchagua viongozi kwa misingi ya dini, kabila na hata ukanda. Bahati mambo haya yameanza kujitokeza katika kampeni za vyama vikubwa zaidi yaani Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ule muungano wa vyama vinne unaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).", "\u00a0", "Watu wanaojihusisha na mambo hayo wanapaswa kuacha mara moja na badala yake watangulize maslahi mapana ya taifa na kuweka pembeni matakwa yao ya madaraka.", "\u00a0", "Hatukubaliani na vitendo hivyo viovu vya kuwania madaraka kwa kutumia mbinu zisizofaa ambazo zinaweza kuitumbukiza nchi katika mtafuruku na hata umwagaji damu.", "\u00a0", "Kuna taarifa za baadhi ya wagombea kupiga kampeni kwa misingi ya ukabila na ukanda na wengine kutumia nyumba za ibada za dini ili kujipigia debe kwa misingi ya imani waliyonayo.", "\u00a0", "Hili jambo halikubaliki hata kidogo, tunaiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kusimamia na kudhibiti kampeni za vyama ili zizingatie sheria za nchi, kanuni za uchaguzi, lakini jambo kubwa zaidi ni kuhakikisha amani ya nchi inadumishwa. Pia Nec inapaswa kukemea na kuchukua hatua madhubuti dhidi ya vyama na wagombea wanaotumia dini, kabila na ukanda kupiga debe ili kupata uongozi wa nchi.", "\u00a0", "Sote tunafahamu kuwa kampeni zinazofanywa kwa misingi ya kibaguzi, zinaweza kuligawa Taifa na kusababisha mgawanyiko unaoweza kuleta maafa makubwa.", "\u00a0", "Nec haipaswi kulifumbia macho vitendo hivi na badala yake ichukue hatua madhubuti dhidi ya wanaofanya kampeni kinyume cha maadili.", "\u00a0", "Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, walioongoza mapambano ya kudai uhuru na walipopewa madaraka, waliweka misingi mema ya amani na utulivu na kulifanya taifa hili kuwa la mfano duniani. Kuna mifano mingi ya nchi ambazo zimetumbikia kwenye machafuko kutokana na athari za migawanyiko ya dini, kabila na kanda. Wagombea wanapaswa kurejea yaliyotokea Kenya mwaka 2007 wakati hisia za kikabila zilipotawala kwenye kampeni za uchaguzi zilipotawaliwa na ukabila na kuibuka ghasia zilizobabisha vifo vya watu takriban 1,500.", "\u00a0", "Pia kuna mfano wa nchi jirani ya Rwanda, mwaka 1994 iliingia katika machafuko makubwa ya vita vya kikabila na kusababisha mauaji ya watu zaidi ya milioni moja.", "\u00a0", "Nchi nyingine ni kama Sudan Kusini na Somalia ambazo zimekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi vikiwa vimesababishwa na dini na ukabila.", "\u00a0", "Pia wananchi wanapaswa kujiweka mbali na watu wanaotumia ukabila, udini na ukanda kujipigia debe ili kupata nafasi ya kuongoza nchi. Ni kwa misingi hii, ndipo tunapowasihi wagombea wa nafasi zote za uongozi, kuhakikisha kwamba kampeni zao zinafaywa kwa kunadi sera za vyama vyao badala ya kuhubiri udini, ukabila na ukanda."], "byline": ["Na Editor \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Tusikaribishe udini wala ukabila kwenye kampeni."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84125", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:05.985747"},
{"body": ["Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati imeteketeza bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu zenye thamani ya Sh. milioni 20.", "\u00a0", "Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kazi ya uteketezaji jana mjini hapa, Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Kati, Fredrick Luyangi, alisema bidhaa zilizoteketezwa zina uzito wa tani 4.4.", "\u00a0", "Luyangi alisema bidhaa hizo ni dawa tani 0.44, chakula tani 3.08 na vipodozi uzito wa tani 0.93.", "\u00a0", "Aidha, TFDA imewaonya wafanyabiashara kuacha kuuza bidhaa zisizofaa, zilizoisha muda wa matumizi na pia vipodozi vyenye viambata vilivyopigwa marufuku baada ya kuonekana kuwa vina sumu.", "\u00a0", "\"Wafanyabiashara wote wanatakiwa kuzingatia kanuni na sheria ili wauze dawa, vyakula na vipodozi vinavyofaa kwa matumizi ya binadamu,\" alisema.", "\u00a0", "Aliongeza vilevile kuwa wananchi wanapaswa kuepuka matumizi ya vyakula, dawa na vipodozi ambavyo vimeisha muda wake na ambavyo havijasajiliwa nchini."], "byline": ["Na Jacqueline Massano\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["TFDA Dodoma yateketeza bidhaa feki za Mil. 20/- ."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=81036", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:06.308616"},
{"body": ["Katika kipindi cha miaka mitano sasa, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ubovu wa mashine ya kipimo cha CT-Scan.", "\u00a0", "Kipimo hiki hutumika kupima mwili wa binadamu kubaini aina mbalimbali ya magonjwa yanayomsibu.", "\u00a0", "Hata hivyo, mara nyingi imekuwa ikiripotiwa kuhusu ubovu wa kifaa hiki na kuwafanya wagonjwa kulazimika kwenda katika hospitali binafsi kupata huduma.", "\u00a0", "Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ni kubwa kuliko zote nchini, kimsingi ni tegemeo la wananchi wengi kwa miaka mingi sasa.", "\u00a0", "Pamoja na jitihada kubwa za serikali katika kuboresha hospitali hiyo, lakini bado kuna maeneo ambayo yamekuwa na matatizo kwa miaka mingi sasa.", "\u00a0", "Katika kipindi cha kati ya miaka minne hadi mitano, imekuwa ikiripotiwa habari ya kuharibika kwa kipimo hicho cha CT-Scan katika Hospitali ya Taifa Muhimbili huku jitihada za kukabiliana na hali hiyo zikiwa ndogo.\u00a0", "\u00a0", "Kitendo cha kuharibika mara kwa mara kwa kifaa hicho kunazua maswali mengi na hasa kutokana na kuwaumiza wananchi ambao hulazimika kwenda kwenye hospitali nyingine kufuata huduma za CT-Scan na hivyo kuingia gharama kubwa.", "\u00a0", "Tunaishauri serikali kutilia mkazo suala hili kwa kuhakikisha matengenezo ya kifaa hiki muhimu katika hospitali hii kubwa ambayo ni kimbilio la Watanzania wengi kwa sasa.", "\u00a0", "Aidha, kutokana na kuharibika mara kwa mara kwa kifaa hicho, yapo mawazo kwamba sasa kuna umuhimu wa kununua CT-Scan nyingine kwa ajili ya hospitali hiyo.", "\u00a0", "Kwa mujibu wa uchunguzi tuliofanya, bei ya CT-Scan ni kati ya Dola 95,000 (sawa na Sh. milioni 201 ) na Dola 165,000 za Marekani (sawa na Sh. bilioni 3.5).", "\u00a0", "Ni dhahiri kwamba bei ya kifaa hicho ni kubwa, lakini tunaamini kuwa serikali ikipanga vipaumbele vyake sawasawa, basi ina uwezo wa kununua CT-Scan kwa ajili ya Hospitali ya Muhimbili kwani `kupanga ni kuchagua.\u2019", "\u00a0", "Tunasema kwa hakika umefika wakati kwa viongozi wa serikali kulipa umuhimu suala hili ili kwa kuamua kununuliwa kwa CT-Scan ili kuwaondolea wagonjwa usumbufu wanaoupata.", "\u00a0", "Tunaamini serikali ikiamua inaweza kwani kifaa kimoja cha CT-Scan kinakaribiana kabisa na bei moja ya gari la aina ya Nissan Patrol, maarufu kama `mashangingi', yaliyotapakaa katika kila wizara, ofisi za serikali na hata halmashauri mbalimbali mikoani.", "\u00a0", "Kwa hakika tunajiuliza, kama uwezo wa kununua mashangingi lukuki tunao, tunashindwaje kununua CT-Scan?.", "\u00a0", "Achilia mbali fedha za kununua mashangingi, pia fedha zinazoelekezwa kwenye semina, warsha, makongamano, safari na shughuli zile kama vile za Siku ya Maji na nyingine ambazo zimekuwa zikigharimiwa kwa mamilioni ya fedha za serikali zinaweza zikaelekezwa kununulia kifaa hicho muhimu.", "\u00a0", "Ikumbukwe kwamba Taifa liko katika vita dhidi ya maadui watatu yaani ujinga, umaskini na maradhi.", "\u00a0", "Tunaiomba serikali ione umuhimu wa kufanya haraka kutengeneza mashine hiyo ya CT-Scan ama kuamua kununua nyingine mpya ili kuokoa maisha ya Watanzania wengi."], "byline": ["Na Editor \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Tatizo la kifaa cha CT-Scan Muhimbili lishughulikiwe."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84188", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:06.719942"},
{"body": ["Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamelalamikia kupanda kwa bei za bidhaa katika masoko baada ya kuanza kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.", "\u00a0", "NIPASHE ilitembelea masoko ya Manispaa ya Temeke, Ilala na Kinondoni na kuzungumza na wafanyabiashara pamoja na wanunuzi ambao kwa nyakati tofauti walizungumzia hali hiyo.", "\u00a0", "Seif Mlanzi mfanyabiashara katika soko la Tandika lililopo Manispaa ya Temeke, alisema bidhaa kama magimbi, mihogo, viazi vitamu na tambi ndizo zilizopanda zaidi kutokana na kutumika zaidi kwa futari.", "\u00a0", "\u201cAwali bei ya magimbi ilikuwa Shilingi 50,000 ila kwa sasa imepanda mpaka kufikia Shilingi 65,000 kwa gunia lenye ujazo wa kati hivyo kusababisha sisi kuuza fungu kwa Shilingi 1,000 mpaka 1,500 tofauti na bei ya awali ya Shilingi 500 kwa 1,000,\u201d alisema Mlanzi.", "\u00a0", "Naye Siajab Jongo mnunuzi wa bidhaa katika soko hilo alisema ameshitushwa zaidi na mfumuko huo wa bei hususani kwa bidhaa zinazotumika kwa futari kitu kinachosababisha hali ya maisha kubadilika.", "\u00a0", "\u201cHali hii inatisha sana ukizingatia ndio siku za kwanza, lakini mambo yashaanza kuwa magumu, bado sielewi ikifikia mfungo 10 na kuendelea mambo yatakuwaje?\u201dalihoji Jongo.", "\u00a0", "Aliongeza kuwa bei ya tambi imepanda kutoka Sh. 1,800 mpaka 2,000 kwa kilo jana kisha kupanda mpaka 2,500 kutoka 2,000.", "\u00a0", "Wakati hali ikiwa si shwari katika soko la Tandika, NIPASHE ilifika katika soko la Stereo lililopo katika manispaa hiyo hiyo na kukuta hali ikiwa haitofautiani sana kutokana na bei za bidhaa mbalimbali za chakula hususani futari kupanda ingawa si kwa kiwango kikubwa.", "\u00a0", "Mshamu Hamis, mfanyabiashara katika soko hilo, alisema bidhaa zilizopanda zaidi ni viazi vitamu huku magimbi yakiwa ndiyo yanaongoza kutokana na bei kupanda kwa kiwango kikubwa wakati awali bei ya kisado ilikuwa Sh. 3,500 na kupanda mpaka 5,000 huku ndoo ikiuzwa kwa Sh. 15,000 badala ya Sh. 10,000 bei ya awali.\u00a0", "\u00a0", "Amina Said, mnunuzi wa bidhaa za chakula katika soko hilo, alilamikia hali hiyo huku akishangaa kutokana na bai kupanda siku chache baadha ya kuanza kwa mfungo tofauti za miaka mingine ambayo bei huanza kupanda kuanzia mfungo wa tao na kuendelea.", "\u00a0", "Katika soko la Tandale lililopo Manispaa ya Kinondoni, bei zilizopanda zaidi ni magimbi na wafanyabiashara waliozungumza na NIPASHE walisema chanzo cha kupanda kwa bei hizo ni kutokana na bei ya jumla kupanda kutoka Sh. 40,000 mpaka 65,000 kwa gunia lenye ujazo wa kati huku ujazo wa juu ikiwa ni Sh. 100,000 bei ya awali mpaka 115,000 bei ya sasa.", "\u00a0", "Upandaji huo wa bei kwa bidhaa hizo ndio uliosababisha wafanyabiashara kupandisha bei kwa mauzo ya rejareja ili kukwepa hasara wanayoweza kuipata kutokana na bei ya jumla kupanda.", "\u00a0", "Aidha bidhaa nyingine zilizopada bei kwa kiwango cha kati katika soko hilo ni tambi, viazi vitamu na mihogo ambazo hata hivyo hazikulalamikiwa sana na wanunuzi.", "\u00a0", "Wakati hayo yakiendelea katika masoko ya Tandale, Tandika na Stereo hali katika soko la Buguruni iko tofauti kwani bei za bidhaa mbalimbali bado hazijapanda huku baadhi ya wafanyabiashara na wanunuzi wakidai huenda mambo yakabadilika siku za usoni.", "\u00a0", "\u201cKwa leo bado ni zile zile ingawa lolote laweza kutokea maana bado mapema sana hivyo hatuwezi kuwa na uhakika moja kwa moja ukizingatia hizi ni siku za mwanzoni tu za mfungo,\u201d alisema Mwanakombo Hamisi, mfanyabiashara katika soko hilo."], "byline": ["Na Waandishi wetu \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Bei ya vyakula yapaa Dar."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=81500", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:07.227715"},
{"body": ["Yapo matukio mabaya ambayo hayajengi jamii ya Watanzania katika kipindi hiki cha kampeni na kuelekea Uchaguzi Mkuu, matukio ambayo kama hayatakemewa na kukomeshwa yanaweza kuwagawa wananchi na kuhatarisha umoja, mshikamano pamoja na amani ya nchi.", "\r\n", "\r\nTumeshuhudia viongozi wa vyama vya siasa wakinadi sera zao kwa wananchi katika hatua za kutoa ushawishi ili wapigiwe kura ifikapo tarehe 25 Oktoba mwaka huu, aidha tumeshuhudia vitendo vya ushabiki kutoka kwa wafuasi wa vyama vilivyoashiria kujenga chuki, fitina na uhasama.", "\r\n", "\r\nWakati hali ya kushabikia wagombea pamoja na vyama vyao inazidi kushamiri, Jeshi la Polisi nchini limewataka wananchi kufuata sheria na kuweka uzalendo mbele ili kuhakikisha kuwa kampeni za Uchaguzi Mkuu zinafanyika kwa amani bila misuguano mikubwa baina ya polisi na raia.", "\r\n", "\r\nPolisi wana majukumu ya msingi ya kuhakikisha usalama wa raia wote pamoja na mali zao, majukumu hayo yanaweza kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa kama wananchi watatoa ushirikiano kwa kufuata sheria zilizopo.", "\r\n", "\r\nSheria zimewekwa ili wananchi wajue ukomo na mipaka inayoweza kuepukwa kwa vurugu na hatimaye kutoweka kwa amani, ukomo huo ni pamoja na kuheshimiana na kukubaliana kwa hoja bila kuwapo na mitafaruku inayoweza kuepukika.", "\r\n", "\r\nWakati mikakati ya kuimarisha umoja wa kitaifa kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu inaendelea, zipo taarifa kuwa wafuasi wa vyama vya CCM na Chadema huko Tarime wamepigana mapanga na kusababisha mmoja wao kupoteza maisha.", "\r\n", "\r\nChanzo cha vurugu hizo inasemekana ni ushabiki ambao inadaiwa kuwa msafara wa mgombea udiwani Kata ya Nyanungu, Mang'enyi Ryoba Masyaga, uliokuwa umeambatana na mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini John Heche, kuvamiwa na wafuasi wa CCM na kusababisha kifo cha Mwita Bhoke.\u00a0\u00a0 ", "\r\n", "\r\nKatikati ya wiki hii, Msemaji wa jeshi la Polisi, Advera Bulimba, alitoa wito kwa Watanzania wote wanaoshiriki kwenye kampeni kuwa wanapaswa kuweka mbele utaifa badala ya ushabiki wa kisiasa unaoweza kuvuruga amani.", "\r\n", "\r\nWananchi wote tunatakiwa kushirikiana kulinda amani yetu, na hilo linawahusu zaidi wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa ambao wanatakiwa kutambua kwamba Utanzania na umoja wetu ndilo jambo linalotakiwa kupewa kipaumbele cha kwanza.", "\r\n", "\r\nTunaamini kuwa misingi imara ya kulinda na kuimarisha umoja wetu wa kitaifa ni urithi mkubwa tuliowekewa na waasisi wa taifa hili, siyo jambo zuri tukakiuka maadili hayo mema kutokana na ushabiki wa kisiasa, kwani tunaelewa kuwa uchaguzi mkuu utapita na Watanzania tutaendelea kuishi tukiwa wamoja. ", "\r\n", "\r\nKujiingiza kwenye ushabiki wa kisiasa uliopitiliza na ambao unaweza ukasababisha uvunjifu wa amani ni kujiingiza kwenye makosa ya jinai, ikumbukwe kuwa sheria zinazosimamia uchaguzi hazitoi mwanya kwa wanasiasa kufanya mambo yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.", "\r\n", "\r\nTunaamini kuwa jeshi la polisi limejiandaa vyema kuhakikisha kuwa amani inadumishwa wakati wote wa kampeni hadi uchaguzi mkuu na mpaka wakati wa kutangazwa kwa matokeo.", "\r\n", "\r\nKwa kutambua na kuthamini amani katika kipindi hiki, Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na jeshi la Polisi, liliandaa mafunzo maalumu kwa maofisa wa polisi yaliyolenga kuwajengea uwezo katika utendaji wao wa kila siku hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi.", "\r\n", "\r\nUNDP tayari limeendesha mafunzo kuhusu uchaguzi kwa vikundi mbalimbali muhimu vikiwemo vya watendaji wa mahakama, wanahabari na polisi. ", "\r\n", "\r\nNaibu Kamishna wa Polisi, Mary Nzuki, mwanzoni mwa wiki hii alisema jeshi hilo limechukua tahadhari zote ili kuhakikisha kuwa kampeni za uchaguzi na uchaguzi wenyewe vinafanyika kwa amani.", "\r\n", "\r\nNi wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha kuwa anakuwa mshiriki mkubwa wa kuimarisha amani pamoja na utulivu wa taifa katika kipindi hiki cha uchaguzi, tofauti zetu kiitikadi zisiwe chanzo cha kuingia katika ushabiki unaoweza kuibua ugomvi na mifarakano.\u00a0 "], "byline": ["Na Mhariri \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Kipaumbele kiwe utaifa, siyo ushabiki wa siasa"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84272", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:07.697902"},
{"body": ["Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima, amewaangukia wakazi wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani akiwataka wasikurupuke kupiga kura za chuki dhidi ya CCM katika uchaguzi mkuu hata kama kuna malalamiko yanayotokana na ubovu wa kimfumo.", "\r\n", "\r\n\"Nawaombeni sana wakazi wa Mkuranga msipige kura za chuki ama hasira dhidi ya CCM; kama kuna matatizo yaliyojitokeza tutayashughulikia na kuyamaliza baada ya kumalizika uchaguzi mkuu. ", "\r\n", "\r\nMpigieni kura nyingi mgombea urais wa chama chetu Dk. John Magufuli na wagombea ubunge na udiwani...Hao wapinzani wetu walioibukia Ukawa na kuichafua CCM nao ni sehemu ya ubovu wanaoulalamikia,\" alisema.", "\r\n", "\r\nAlisema mgombea urais anayepeperusha bendera wa vyama vinavyounda Ukawa, kupitia Chadema ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Fedrick Sumaye, wanahubiri kwamba CCM ni mbovu lakini wamesahau kuwa wao ndio walioifikisha hapo kwa kuitengenezea majeraha ya kila namna.", "\r\n", "\r\nMalima alikuwa akizungumza jana katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan, uliofanyika kijiji cha Kimanzichana Wilaya ya Mkuranga.", "\r\n", "\r\nKwa upande wake, mgombea mwenza wa Suluhu akizungumza na wananchi hao, alisema iwapo Dk. Magufuli atapata ridhaa ya kuunda serikali ya awamu ya tano anawaahidi kujenga kiwanda cha kisasa cha kubangua korosho katika Wilaya ya Mkuranga.", "\r\n", "\r\n\"Tuchagulieni Dk. Magufuli na wagombea ubunge na udiwani ili tulete maendeleo Mkuranga. Tumejipanga na tunaahidi kujenga kiwanda cha kubangua korosho hapa kwenu. Ujenzi huu pia utafungua fursa za ajira kwa vijana lakini pia kitaongeza kipato cha wakazi wa Mkuranga na maeneo ya jirani,\" alisema Samia.", "\r\n", "\r\nAlisema nia ya serikali ijayo ya CCM ni kuwawezesha wakulima wa zao hilo kufungasha zao hilo katika njia ya kisasa na kuuza kwa tija ndani na nje ya nchi.", "\r\n", "\r\nAlisisitiza kuwa Dk. Magufuli na serikali yake atakayoiunda iwapo atapata ridhaa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu; ameahidi pia kujenga soko kuu la zao la korosho ambalo litakuwa mkombozi wa wakulima wa zao hilo nchini."], "byline": ["Na Godfrey Mushi\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Malima awaangukia Mkuranga"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84267", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:08.041328"},
{"body": ["Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, amesema kuwa,\u00a0 elimu bure kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu, itawezekana, ikiwa kiongozi ajae atabadilisha mfumo wa ukusanyaji kodi kwa kuwabana wafanyabiashara wakubwa ambao wamekuwa wakilalamikiwa kutoilipa.", "\r\n", "\r\nWakati Mukoba akiyasema hayo, mgombea Urais Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ameahidi atakapoingia madarakani, atahakikisha elimu inatolewa bure kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu.", "\r\n", "\r\nMgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, kupitia ilani yao wanayoinadi hivi sasa, imeahidi elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu.", "\r\n", "\r\nKatika mahojiano na Nipashe Jumapili, Mukoba alisema elimu bure ilikuwa inawezekana kwa kipindi kirefu lakini tatizo lipo katika mfumo wa uongozi.", "\r\n", "\r\nAlisema fedha nyingi zimeelekezwa sehemu tofauti huku sekta ya elimu ikibaki kuwa na changamoto.", "\r\n", "\r\n\u201cTunapoambiwa elimu bure ninavyoelewa mimi ni kwamba fedha za kuendesha sekta hii na nyingine zitatokana na kodi zetu,\u201d alisema na kuongeza:", "\r\n", "\r\nAlisema ikiwa mfumo wa ukusanyaji kodi wa sasa utaendelea kama ulivyo, suala la elimu bure halitawezekana.", "\r\n", "\r\n\u201cNchi kama Botswana kule wanachimba madini na mwekezaji kwenye sekta hiyo anatoa asilimia 50 serikalini, Ghana wao wamefanikiwa kuwaboreshea walimu mishahara yao, kwa nini sisi tushindwe,\u201d alihoji.", "\r\n", "\r\nAliongeza kuwa, walivyokwenda kupanua elimu kimataifa walikubaliana watenge pato la ndani la taifa asilimia sita, lakini Tanzania haijawahi kutenga hata asilimia mbili.", "\r\n", "\r\nAlimtaka kiongozi ajae atoe kipaumbele cha kwanza katika elimu kwa kuhakikisha changamoto za vitendea kazi, maabara, walimu na upungufu wa madawati vinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.", "\r\n", "\r\nNaye, Mkuu wa Kitengo cha Sayansi na Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, akitoa maoni yake, alisema suala hilo litawezekana ikiwa litatekelezwa kwa awamu.", "\r\n", "\r\nAlisema kama walivyoanza na shule za msingi, baadaye wanatakiwa kwenda mbele zaidi kwenye shule za sekondari na kumalizia chuo kikuu.", "\r\n", "\r\n\u201cKama watatoa elimu bure na kuibana sekta nyingine kwa kuiongezea malipo ili kufidia, itawekana. Ila wanaoahidi wanatakiwa kufanya uchunguzi wa kutosha kwenye ahadi hii na kuwaeleza Watanzania vyanzo vya mapato vya ziada watavipata wapi,\u201d alisema."], "byline": ["Na Romana Mallya\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Mukoba: Elimu bure nchini inawezekana, kodi zikusanywe"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84265", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:08.228051"},
{"body": ["Rais Jakaya Kikwete, ameijia juu Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na menejimenti yake akiitaka kufanya utatifi zaidi kuhusu mambo ya kale katika hifadhi hiyo ili yaweze kuongeza mazao zaidi ya kuvuta watalii wengi badala ya wanyama na kreta pekee.", "\r\n", "\r\nAkiweka jiwe la msingi jana la jengo la kitega uchumi la NCAA litakalokuwa na ghorofa 15\u00a0 katikati ya Jiji la Arusha, Rais Kikwete alisema wakati nchi zingine kama Misri na Afrika Kusini zikiendelea na tafiti za mambo ya kale, wataalam wa Tanzania (Ngorongoro) wameacha kufanya utafiti.", "\r\n", "\r\nAlisema kwa mfano utafiti wa nyayo za binadamu wa kwanza kama ulivyofanywa na Dk. Leakey, haujaendelea tena na hata uhifadhi wa nyayo hizo kama ulivyo sasa unahatarisha kupoteza ushahidi wa uvumbuzi huo.", "\r\n", "\r\n\u201cNgorongoro haiwezi kuishinda Serengeti inapokuja suala la wanyama\u2026watalii wengi wanapenda kupita Ngorongoro sio kuangalia wanyama bali vivutio kama kreta yenye wanyama, mchanga unaotembea na historia ya mambo ya kale,\u201d alisema na kuongeza, \u201clazima akili ibadilike na kuongeza bidhaa zaidi ya wanyama.\u201d", "\r\n", "\r\nHata hivyo, aliipongeza NCAA kwa kubuni kitega uchumi kwa kuamua kujenga jengo hilo litakalokuwa la ghorofa 15.", "\r\n", "\r\nAlisema jengo hilo lililopewa jina la Jakaya Kikwete Ngorongoro Tower, litapendezesha taswira ya jiji la Arusha.", "\r\n", "\r\nMapema Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Mahmood Mgimwa, alimpongeza Rais Kikwete kwa kufanya ziara za kikazi mara nyingi na zile za mapumziko katika Hifadhi ya Ngorongoro, jambo ambalo limekuza kwa kiasi kikubwa utalii wa ndani.", "\r\n", "\r\n\u201cHivi sasa wananchi wengi nchini pamoja na familia zao wameanza kuhamasika kuja na kutembelea hifadhi hii ya kwa ajili ya kujiburudisha na kujifunza hifadhi ya mazingira, maisha na tabia mbalimbali za wanyamapori wanaopatikana katika Hifadhi ya Ngorongoro,\u201d alisema.", "\r\n", "\r\nAkitoa taarifa kuhusu jengo hilo kwa Rais Kikwete, Mwenyekiti wa Bodi ya NCAA, Balozi Mwanaidi Maajar, alisema gharama za ujenzi wa jengo hilo hadi kukamilika kwake Novemba mwakani itakuwa zaidi ya Sh. bilioni 42.3."], "byline": ["Na John Ngunge\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Rais Kikwete aijia juu NCAA"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84266", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:08.611222"},
{"body": ["Mamkala ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), juzi ilitangaza kupokea mapendekezo ya nauli kutoka kwa Wakala wa Mabasi ya Mwendo Kasi Dar es Salaam (Dart).", "\u00a0", "Mapendekezo ya nauli hizo yanatazamiwa kutumiwa na kampuni ambayo itatoa huduma ya usafiri wa umma katika njia na miundombinu ya Dart katika kipindi cha mpito.", "\u00a0", "Kiwango cha juu kilichopendekezwa na Dart ni Sh. 900 ambacho kitahusu zaidi safari katika njia za pembezoni na njia kuu zilizojengwa kwa ajili ya kutumiwa na mabasi hayo.", "\u00a0", "Pia viwango vingine vilivyopendekezwa ni Sh. 700 na Sh 500, viwango vinavyotegemea zaidi njia inayotumiwa na wananchi. Kufuatia mapendekezo hayo, Sumatra imetangaza kuwa itakaa na wadau kujadiliana nayo juu ya mapendekezo hayo ya nauli kama yalivyotolewa na Dart.", "\u00a0", "Hata hivyo, mapendekezo hayo tayari yamezua manung\u2019nuko kutoka kwa wananchi ambao wanaamini kuwa kiasi kilichopendekezwa ni kikubwa kuliko hali halisi ya kiuchumi. Ni dhahiri kwamba usafiri wa mabasi ndiyo tegemeo kubwa kwa wananchi wa kipato cha chini katika Jiji la Dar es Salaam, hivyo kupanga kiasi kikubwa cha nauli kwa vyovyote vile kitawaathiri kwa kiasi kikubwa.", "\u00a0", "Tunaiomba serikali iangalie suala hili la nauli kwa kuwa tunaamini kwamba uanzishwaji wa mradi wa Dart ulikuwa na nia njema ya kuwapunguzia adha wakazi wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na kupunguza foleni.", "\u00a0", "Mradi wa Dart ulianzishwa kufuatia mkopo wa Dola milioni 290 za Marekani kutoka Benki ya Dunia ambao Serikali ya Tanzania itatakiwa kuulipa. Kwa maneno mengine ni kwamba fedha za umma zitatumika kulipa mkopo wa mradi huo.", "\u00a0", "Kwa msingi huu, wananchi wengi walikuwa na matumaini kwa kuwa fedha zinazotumika ni za mlipa kodi, kutakuwa na nafuu tofauti na usafiri wa mabasi ya daladala yanayomilikiwa na sekta binafsi. Lakini katika hali ya kushangaza, mapendekezo ya Dart yanatoa picha kuwa mradi huu unaelekea kujiegemeza \u00a0katika kutengeneza faida zaidi badala ya kusaidia wananchi wa kipato cha chini waliokuwa wakiisubiri kwa hamu huduma hii. Uzoefu unaonyesha kwa mifano ya nchi mbalimbali duniani kuwa pale serikali inapoweka mkono katika uendeshaji wa usafiri wa umma, nauli zake ni nafuu.", "\u00a0", "Kitendo cha Dart cha kutaka kutoza nauli za kiasi kikubwa, kitawaumiza wananchi wa kawaida ambao katika wakati huu tayari wana hali ngumu ya maisha ikichangiwa na uduni wa uchumi unaochangiwa kuporomoka kwa thamani ya Shilingi kwa kiasi kikubwa kutoka kwa dola siku za karibuni.", "\u00a0", "Ni matumaini yetu kuwa Sumatra itasikiliza kilio cha wananchi walio wengi na kuhakikisha kuwa wanapanga bei za usafiri wa mabasi ya Dart zinazoendana na uhalisia wa maisha ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wa kipato cha chini.", "\u00a0", "Aidha, kwa Dart kupendekeza kiwango hicho cha juu cha nauli, kunaweza kuamsha kilio kutoka kwa wamiliki wa mabasi ya daladala ambao kila mara nao wamekuwa wakililia kupandishwa kwa nauli kwa kisingizio cha kupanda kwa gharama za uendeshaji.", "\u00a0", "\u00a0Tunaomba wadau kujitokeza kwenye mkutano wa kujadili mapendekezo hayo ya nauli za mabasi ya Dart ulioandaliwa na Sumatra ili upatikane muafaka utakaokidhi matakwa ya wananchi wanaolilia usafiri wa uhakika na wa bei nafuu.", "\u00a0"], "byline": ["Na Editor \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Nauli za mabasi ya kasi zipangwe kuzingatia kipato cha wananchi."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84157", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:09.232639"},
{"body": ["Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juzi lilisaini mkataba wa miaka minne na Kampuni ya Azam Media wenye thamani ya Sh. bilioni 3.3 kwa ajili ya kudhamini mashindano ya Kombe la FA yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba mwaka huu.", "\u00a0", "Michuano hiyo ambayo kwa mara ya mwisho ilifanyika 2002 na timu ya JKT Ruvu Stars ya Pwani kutwaa ubingwa kwa kuifunga Baker Rangers ya Magomeni katika fainali, inakuja kuleta kitu kile ambacho Nipashe tunaamini kama itafanikishwa kitainua soka la nchi hii.", "\u00a0", "Kwa nchi kama ya Tanzania ambayo hamna msingi wa soka, ni ngumu kupata vipaji vipya kama hamna mashindano ya kutosha.\u00a0", "\u00a0", "Ni kupitia michuano kama hiyo ambayo inashirikisha hadi timu za mitaani ndiko vipaji vinaweza kuonekana.", "Ingawa kwa sasa michuano hiyo inayoanza Novemba mwaka huu itashirikisha timu 64 tu kutoka madaraja matatu ya juu ya soka, lengo la kuja kushirikisha hadi timu za mitaani ndilo la msingi zaidi.", "\u00a0", "Kwasababu wachezaji wa ligi za juu tayari wanapo mahali pa kuonekana na kuonyesha vipaji vyao, kupitia michuano kama ya Kombe la FA ni fursa kubwa kwa wasio na 'jukwaa' la kuonyesha uwezo wao.\u00a0", "\u00a0", "Timu za mchangani, kwa mfano, zitakapoanza kushiriki zitapata \u2018jukwaa\u2019 la kuonyesha \u2018majembe\u2019 yao yote. Kipa wao chaguo la kwanza atacheza, beki, kiungo na mshambuliaji kila mmoja atapata nafasi ya kuonyesha uwezo wake dhidi ya timu kubwa, pengine, ambayo watapangwa kucheza dhidi yao.", "\u00a0", "Hizi ndizo fursa ambazo Nipashe tumekuwa tukizipigia kelele kwa miaka mingi. Siyo michuano ya \u2018kisiasa\u2019 ya Kombe la Taifa.", "\u00a0", "Michuano ya \u2018kisiasa\u2019 ya Kombe la Taifa ambayo TFF hii pia ilipata kueleza ndoto yake ya kuirejesha, haina maana yoyote.", "\u00a0", "Kwa taifa ambalo halitaki kuruhusu mgawanyiko wowote wa kitabaka, kikanda, au mwingine wowote ni wazi kwamba michuano ya Kombe la Taifa haina manufaa.", "\u00a0", "Kwa sababu ya kuhofia kuwagawa Wazaramu pekee wachezee timu ya mkoa wa Dar es Salaam, kwa mfano, na Wachaga tu wachezee timu ya mkoa wa Dar es Salaam, kanuni za mashindano ya Kombe la Taifa zimekuwa zikiruhusu mchezaji wa mwenye asili ya mkoa wowote kuchezea mkoa mwingine wowote.", "\u00a0", "Uchache wa mikoa unamaanisha kwamba ni wachezaji wachache sana watakaopata fursa ya kucheza. Na mbaya zaidi kwa wachezaji vijana wanaotaka kuonyesha vipaji vyao hawawezi kupata fursa hiyo kwa sababu makocha wa timu za mikoa hawafungwi kuchagua nyota wakubwa na matokeo yake michuano inatawaliwa na wachezaji walewale wanaoonekana kwenye TV \u2013 wa Ligi Kuu.", "\u00a0", "Matokeo yake mantiki hasa ya michuano hiyo haionekani. Kama unawaona kina Ramadhani Singano, Simon Msuva kwenye mechi za Ligi Kuu, ina maana gani tena kuwaona wamejaa peke yao katika michuano ya Kombe la Taifa?", "\u00a0", "Kwa sababu makocha wa timu za mikoa wanataka kuitumia michuano hiyo kutengeneza \u2018CV\u2019 zao, ni ngumu kwao kuwatumia wachezaji yosso wasiojulikana. Matokeo yake wanajaa nyota wa ligi kuu tu.", "\u00a0", "Lakini michuano ya Kombe la FA, inazipa fursa timu hata za mchangani kuwatumia nyota wao wote na kuonyesha vipaji vyao. Ni kwa namna hiyo unaweza kuona vipaji vipya, si kwa kuangalia nyota walewale wa Simba, Yanga na Azam."], "byline": ["Na East africa radio \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Kombe la FA lifute mawazo mabaya ya Kombe la Taifa."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84219", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:09.612993"},
{"body": ["Mgombea udiwani kata ya Ibinzanamata kupitia Chama Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Siaba Kakema, amesema kituo cha kulea na kutunza watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) cha Buhangija, kimesahaulika na kukosa huduma za kibinadamu ikiwemo chakula.", "\r\n", "\r\nAlisema hali hiyo inatokana na viongozi kutotoa kipaumbele katika mipango ya maendeleo na watu wenye ulemavu huo kujiona kama wametengwa na jamii.", "\r\n", "\r\nAlisema akiingia madarakani na kuwa mwakilishi wa wananchi wa kata hiyo, atahakikisha wanapata huduma zote muhimu za kibinadamu.", "\r\n", "\r\nAidha, aliahidi kuwatetea albino na kuhakikisha kituo hicho kinapata chakula cha kutosha kutokana na hivi sasa kukabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo watoto waliopo kituoni hapo kukosa chakula huku viongozi wenye dhamana hiyo, wakiponda raha mitaani.", "\r\n", "\r\nAlisema kuwa atawashawishi wadau wote wakiwamo wafanyabishara wa ndani ya eneo lake, kuona kituo hicho kina kuwa mahali sahihi kwa binadamu kuishi badala ya kutengwa na jamii huku maisha yao yakiwa mashakani.", "\r\n", "\r\nKuhusu kuendeleza makundi maalum ya akina mama na vijana, alisema atahakikisha anatumia ilani ya chama chake yenye falsafa ya ya utu, uzalendo na uadilifu, kubadili hali zao kwa kubuni miradi midogo midogo ya ujasiriamali."], "byline": ["Na Anceth Nyahore\n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Mgombea udiwani ACT-Wazalendo atetea albino"], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84268", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:09.623289"},
{"body": ["Shirika la Umeme nchini (Tanesco), juzi lilitangazia umma kwamba nchi nzima itakuwa gizani kwa takriban wiki nzima kuanzia jana.", "\u00a0", "Shirika hilo lilieleza kuwa hali hiyo inatokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi inayozalisha umeme kutoka Songosongo mkoani Lindi.", "\u00a0", "Tanesco ilifafanua kuwa imechukua hatua hiyo kutokana na kazi ya kuunganisha bomba la gesi kutoka Mtwara na mtambo wa umeme wa Kinyerezi II.", "\u00a0", "Aidha, hali ya umeme ilitarajiwa kuwa mbaya zaidi jana kwa kuwa mitambo yote ya kuzalisha nishati hiyo ilikuwa inatarajiwa kuzimwa ili kufanikisha kazi hiyo.", "\u00a0", "Tunaamini kwamba dhamira ya Tanesco ni njema na imelenga kuboresha utoaji huduma umeme nchini ambayo kwa miaka nenda rudi, imekuwa haikidhi matarajio ya wateja wake na Watanzania kwa ujumla.", "\u00a0", "Hata hivyo, sisi hatuamini kuwa hatua ya Tanesco ya kuunganisha bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara na mitambo yake, imekuwa ni ya dharura kiasi cha kulazimika kutoa taarifa kwa umma siku moja kabla.", "\u00a0", "Tunasema na tuna imani kwamba mpango wa shirika hilo wa kuunganisha bomba hilo na mitambo ya Kinyerezi, haukuibuka ghafla tu juzi na hivyo kulazimika kuwapa wateja wake notisi ya muda mfupi, bali lilijipanga kwa kwa muda mrefu kwa kazi hiyo pasipo kukurupuka.", "\u00a0", "Kwa msingi huo, menejimenti ya Tanesco ilipaswa kutoa tahadhari mapema kwa wateja wake juu ya kuwapo kwa hatua ya kuzima mitambo yake ili kuwawezesha kujipanga kukabiliana na tatizo hilo.", "\u00a0", "Ni dhahiri kwamba mamilioni ya watu nchini, hutegemea nishati ya umeme kwa shughuli mbalimbali za kila siku za kujiongezea kipato pamoja na viwanda.", "\u00a0", "Mathalani, ukiachilia mbali viwanda ambavyo kwa asilimia kubwa hutegemea umeme wa Tanesco, lakini pia wajasiriamali mbalimbali hutegemea nishati ya umeme kuendeshea shughuli zao za kiuchumi kama vile saluni za kike na kiume, inateneti, gereji za magari, wauzaji wa vinywaji baridi na vikali, wauza samaki na nyama, mama ntilie, wachomeleaji vyuma; kutaja baadhi.", "\u00a0", "Kwa msingi huo, ni jambo lililo wazi kwamba hatua hii ya Tanesco kwa kiasi kikubwa itaathiri shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii ambazo kwa kiasi kikubwa zinategemea nishati ya umeme.", "\u00a0", "Ni kutokana na hilo, ndipo tupoona umuhimu wa Tanesco ingepaswa kutoa taarifa ya kukosekana kwa umeme mapema zaidi ili makundi hayo yote yajiandae vya kutosha.", "\u00a0", "Kimsingi, Tanesco haikuwatendea haki wateja wake na umma wa Watanzania kwa kufanya uamuzi huo wa ghafla wa kuzima mitambo yake bila kujali athari watakazokumbana nazo.", "\u00a0", "Aidha, hatua hii ya Tanesco kwa kiasi kikubwa pia itaathiri uzalishaji wa viwandani kwani vitalazimika kuingia gharama za kutumia majenereta yanayotumia mafuta.", "\u00a0", "Matumizi ya jenereta, ni wazi kwamba yatachangia kwa kiasi kikubwa kupandisha bei ya bidhaa zinazozalishwa viwandani na hivyo kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.", "\u00a0", "Viwanda vingi vinaendeshwa kwa bajeti na hatua hii ya Tanesco kuzima ghafla mitambo yake, italeta athari kubwa.", "\u00a0", "Mbali na shughuli hizo za kiuchumi, lakini pia kuna masuala ya kijamii kama shughuli za hospitali kwani kwa hatua hii ya Tanesco, ni dhahiri wagonjwa wengi wanaohitaji huduma za matibabu wataathirika.", "\u00a0", "Ikumbukwe kuwa Tanzania kwa sasa inapigania kupeleka watu wake kwenye uchumi wa kati, na kwa msingi huo suala la nishati ya umeme, ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini wanaotaka kuinua hali zao za maisha.", "\u00a0", "Kwa hakika Tanesco inapaswa kukubali kwamba haikuwatendea haki wateja wake na umma wa Watanzania kwa hatua yake hii.", "\u00a0", "Hata hivyo, sisi hatupingi dhamira njema ya Tanesco kuboresha miundombinu ya umeme nchini, tunachosisitiza ni kwmaba yalipaswa kuwapo mawasiliano bora na ya mapema ambayo yangesaidia wananchi kujipanga vizuri na athari za makali ya kukatwa kwa umeme.", "\u00a0"], "byline": ["Na Editor \n\t\t\t\t\t"], "publication": "nipashe", "title": ["Tanesco hamjatenda haki, mngetoa taarifa mapema."], "url": "http://www.ippmedia.com/?l=84094", "scraped_at": "2015-09-14T11:44:10.259664"}]